Monday 25th, January 2021
@Vwawa Mkoani Songwe
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasimu Majaliwa Majaliwa(MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kongamano la uwekezaji Mkoa wa Songwe litakalofanyika 15-17 February 2020 katika Viwanja vya CCM Vwawa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brg. Jen. Nicodemus Mwangela amesema lengo la kongamano la uwekezaji ni kuutangaza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo Mkoa wa Songwe.
"Mkoa tuna fursa ya barabara kuu ya Tanzania na Zambia ambayo 75% ya mizigo inayoshuka bandari ya Dar inapitia Songwe katika mpaka wa Tunduma pamoja na Reli ya TAZARA" Mhe. Mwangela Mkuu wa Mkoa wa Songwe akitaja baadhi ya fursa, 31 Januari 2020.
Pia, Mhe. Mwangela amesema siku ya kongamano Mkoa utazindua kitabu cha uwekezaji yaani 'Songwe Investment Guideline'
Mhe. Mwangela amewataka wananchi, wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uwekezaji na fursa ya uwekezaji.
Kaulimbiu ya kongamano ni wekeza Songwe lango kuu la SADC
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957389
Simu ya Mkononi: +255 754 549 511
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa