• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

MADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA MKOA WA SONGWE YAFANYIKA WILAYANI MOMBA

Imewekwa : June 21st, 2023

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni siku ambayo inakumbukwa na jumuiya yote ya Umoja wa Afrika kutokana na umuhimu wake katika kupigania haki ya elimu bora ya mtoto wa Afrika isiyo na ubaguzi.


Maadhimisho haya yanafanyika ili kuenzi michango ya watoto wa Kiafrika walioshiriki kupinga ubaguzi wa Elimu iliyokuwa inatolewa wakati wa utawala wa Serikali ya Makaburu huko Afrika Kusini. Tarehe na mwezi kama wa leo mwaka 1976, Watoto zaidi ya 100 wa Kiafrika waliandamana kudai Elimu bora na hatimaye waliuawa na askari wa utawala wa Makaburu.


Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka 2023 yanafanyika yakiwa na ujumbe na dhima ya kuelimisha jamii katika kuhimiza Elimu bora na kuacha ubaguzi kwa watoto kwa Kauli mbiu inayosema “ZINGATIA USALAMA WA WATOTO KATIKA ULIMWENGU WA KIDIGITALI”.


Kumbukizi ya tukio hili linatia huzuni na uchungu sana duniani pia lipo jambo la kujifunza na ndiyo maana tunafanya maadhimisho haya kila mwaka. Jambo la huzuni zaidi ni kwamba watoto waliokuwa wawe viongozi wa leo waliuawa kikatili bila kujali matakwa yao. Inauma sana.


Jambo la kujifunza katika kumbukizi siku hii ni umoja, ukomavu wa kifikra na ujasiri wa watoto wa Afrika walioonyesha wakati wanadai haki yao ya msingi ambayo ni elimu bora. Kutokana na jitihada hizo za watoto zikiwemo kutembea zaidi ya nusu maili, kuliamsha hisia za kupinga ubaguzi wa rangi ulimwenguni kote. Umoja wa Nchi huru za Kiafrika (OAU) uliazimia na kupaza sauti ya kupinga ukatili na ubaguzi kwa watoto, juhudi ambazo ziliungwa mkono na Jumuiya za Kimataifa.


Ujumbe katika maadhimisho ya Mtoto wa Afrika mwaka 2023 unatukumbusha wazazi kumlinda mtoto wa “kisasa” dhidi ya ukatili wa kupigwa, kulawitiwa, kukosa elimu, kubaguliwa, kunyanyaswa, kutopata haki zake za msingi na kubwa zaidi ulimwengu wa tunaoita wa kisasa wa matendo maovu yanayopinga uwepo wa Mwenyezi Mungu.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa