• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

'Ahadi Imetimia, Bilioni 119.9 Kutumika Mradi wa Maji Tunduma, Vwawa'

Imewekwa : May 20th, 2025

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameshuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tunduma - Vwawa, Kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri (kwa niaba ya Serikali) na Meneja Mradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya China (China Civil Engineering Construction Corporation-CCECC), Ning Yunfeng.

Tukio hilo limefanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma leo tarehe 20 Machi 2025 ambapo mradi huo kutoka Chanzo cha Maji ya Mto Momba, uliopo Wilaya ya Momba, mkoani Songwe utakaogharimu shilingi bilioni 119.9 za Tanzania.

Mradi huo utahusisha ujenzi wa chanzo cha maji (Intake) chenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 21.5, ujenzi wa Kituo cha kuchakata na kutibu maji chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 20 kwa siku, ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusafirisha maji yenye kipenyo cha milimita 100 yenye urefu wa kilometa 96, ujenzi wa matenki ya maji yenye uwezo wa kuhifadhi ujazo wa lita milioni 5 litakalojengwa katika Mtaa wa Uwanjani/Uhuru, Halmashauri ya Mji Tunduma, tenki la lita milioni 3 litakalojengwa katika Kijiji cha Ikana na tenki lenye ujazo wa lita milioni 2 litakalojengwa katika Kijiji cha Nkangamo, Ununuzi wa pampu, Ujenzi wa Ofisi na Vitendea kazi vingine.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Songwe waliojitikeza kushuhudia tukio hilo katika Uwanja huo mjini Tunduma, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewahakikishia Wananchi hao kuwa Serikali itatoa fedha zote za kutekeleza mradi huo ambao ni ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kumtua mama ndoo kichwani.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso, amempongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi hicho cha fedha takriban shilingi bilioni 120, ambazo ni fedha za ndani, kwa ajili ya kuwaondolea adha ya maji Wananchi wa Tunduma, Vwawa na Mlowo, watakaofikiwa na mradi huo.

 Mradi huo unatarajia kuwanufaisha wakazi 219,309 katika miji hiyo ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18 kukamilika na kuanza kutoa maji safi na salama kwa Wananchi.

Matukio katika Picha:

(Picha zote na Julius Evandino, TTC).

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mei Mosi Songwe Yafana

    May 01, 2025
  • Chaurembo Awapongeza Walimu

    April 30, 2025
  • Tunduma kwa Taaluma Sina Mashaka Nanyi: RAS Seneda

    April 30, 2025
  • Chaurembo Afungua Mafunzo Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili

    April 29, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa