• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Bajeti Zijibu Kero za Wananchi: RC Dkt. Francis

Imewekwa : February 5th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael amezitaka Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha kuwa Bajeti zinazopangwa na kupitishwa na mamlaka hizo zinazingatia matakwa na kero za Wananchi ili matokeo yake yatatue kero zao.

Dkt. Michael amesema hayo wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha mapendekezo  ya mpango na bajeti ya Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 05 Februari 2024.

Kikao hicho kimewahusisha Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Songwe, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri zote 05 mkoani Songwe.

Aidha, Dkt. Michael amezitaka Halmashauri zote ndani ya Mkoa wa Songwe kuepuka migogoro ya ukusanyaji wa mapato na kuweka mikakati thabiti ya kushughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kuwa mapato mazuri ndiyo suluhisho la maendeleo ya miradi na uendeshaji wa Ofisi.

Katika hatua nyingine Mkuu Mkoa huyo amewataka Wataalam katika Halmashauri zote katika Mkoa huo kuwa wabunifu katika makadirio ya makusanyo ya fedha za ndani na kuepuka kuweka malengo madogo ambayo hata wakifikia asilimia 100 bado itakuwa haiakisi uhalisia na ni sawa na kijidanganya wenyewe.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe,  Happiness  Senada  ameweka msisitizo katika utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb), ambapo maagizo hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa  vipaumbele vya bajeti vinajibu hoja za Wananchi, kuweka mikakati ya kukusanya mapato, kudhibiti matumizi ya Mashine za kukusanya Mapato (POS), upelekaji wa fedha katika Miradi ya Maendeleo, kusimamia Miradi  na kuhakikisha inakamilika, Upelekaji wa asilimia 10 kwenye mfuko husika, utekelezaji wa hoja na kudhibiti fedha zinazokusanywa kupeleka benki.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo ameeleza kuwa Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 inakadiriwa kuwa shilingi bilioni 36.3 ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 13,8 ni kutokana na vyanzo vya ndani, shilingi milioni 950.3 kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji (OC), shilingi bilioni 13.2 kwa ajili ya mishahara na shilingi bilioni 8.2 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali Kuu na Wahisani.

Chaurembo amebainisha kuwa pamoja na Vipaumbele vya Halmashauri ya Mji Tunduma, Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umezingatia vipaumbele mbalimbali vya Kisekta kama vile kuimarisha masuala ya Utawala Bora, kuendeleza Watumishi, kuzingatia masuala mtambuka ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, madawa ya kulevya, maambukizi ya VVU na unyanyasaji wa kijinsia.

Ametaja mambo mengine yaliyozingatiwa ni kutenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, kutekeleza Sheria za Mipango Miji kwa kupima na kurasimisha makazi holela na kuandaa Hati Miliki za Ardhi, kuinua kiwango cha ukusanyaji mapato, utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika ngazi za chini kwa kuzingatia asilimia 60 ya vyanzo vya ndani ikijumuisha asilimia 10 ya Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Matukio katika Picha:

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael akisikiliza kwa makini mawasilisho ya Wakurugenzi wa Halmashauri wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 05 Februari 2024.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 05 Februari 2024 ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Francis Michael.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Happiness Seneda (kushoto) wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 05 Februari 2024 ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Francis Michael.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma,  Mariam Chaurembo akiwasilisha vipaumbele vya bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 05 Februari 2024 ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Francis Michael.

Kikao kazi cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 05 Februari 2024 ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Francis Michael.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa