• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Chaurembo: Viongozi wa Dini Tunawategemea

Imewekwa : May 21st, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo amesema Serikali inawategemea Viongozi wa Dini katika kuhamasisha masuala ya lishe katika jamii kwa kuwa wana ushawishi mkubwa kupitia nyumba zao za ibada na jamii inawasilikiliza.

Chaurembo ameeleza hayo alipokuwa akifungua kikao cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 21 Mei 2024.

"Viongozi wa Dini mna mchango mkubwa sana wa kuibadilisha jamii kwa kuwa inawaamini na inawasikiliza...jamii yetu inakabiliwa na changamoto kubwa ya udumavu, niwaombe mnapokuwa kwenye nyumba za ibada tusaidieni kuielimisha jamii kukabiliana na changamoto hiyo kuzingatia suala la lishe kwa jamii hasa watoto."Amesema Chaurembo.

Akiwasilisha Mwongozo wa Utekelezaji wa Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji au Mtaa (SALiKi), Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Tunduma, Frida Muhindi amesema Mwongozo huo ni mkakati ambao umeshirikisha sekta mbalimbali zinazotoa huduma za kinga na tiba ambazo zinahusiana na lishe.

Muhindi amesema Mwongozo huo unatumika kuhamasisha mabadiliko chanya ya tabia zinazohusu afya na lishe katika jamii. Hivyo, Muhindi amesema Mwongozo huo umetayarishwa ili kurahisisha utekelezaji wa afua za lishe katika siku hiyo.

Ameongeza kwa kufafanua kuwa, huduma muhimu za Afya na Lishe ni za lazima katika ukuaji na maendeleo ya watoto walio katika umri chini ya miaka mitano (5), pamoja na jamii kwa ujumla.

 

Afisa Lishe huyo ameongeza kuwa huduma hizo kwa kawaida hutolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo wazazi na walezi walio wengi hawana ufahamu mzuri wa huduma

Ameeleza kwamba SILiKi inatoa fursa kwa wazazi na walezi kupata huduma hizo katika jamii yao pamoja na kupata taarifa sahihi, kubadilishana na mawazo na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika malezi ya watoto.

 Aidha, pamoja na mambo mengine, pia Muhindi aliwasilisha mada kuhusu viashiria, visababishi na madhara ya utapiamlo katika jamii.

Matukio katika Picha:

Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Tunduma, Frida Muhindi akiwasilisha Mwongozo wa Utekelezaji wa Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji au Mtaa (SALiKi) wakati wa kikao cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 21 Mei 2024.

Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Tunduma, Anna Wandwi akizungumza kuhusu umuhimu wazazi na walezi kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto ili kubaini vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa kwa nyakati ambazo wao mbali nao, wakati wa kikao cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 21 Mei 2024.

(Picha zote na Benton Nollo)


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa