• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DC Kihongosi: Zingatieni Usafi Kuepuka Kipindupindu

Imewekwa : January 16th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi amewaasa wakazi wa Tunduma kuzingatia kanuni za usafi ili kujikinga dhidi ya Ugonjwa wa Kipindupindu ambao umethibitika kuwepo katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Mwanza.

Mhe. Kihongosi ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na Wananchi, Wafanyabiashara na Wajasiriamali kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Kihongosi amewataka Wananchi kuzingatia usafi ili kuepuka kipindupindu kwa kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni kabla ya kula kitu chochote na baada ya kutoka chooni, kuweka mazingira ya nyumba na choo katika hali ya usafi wakati wote, kuandaa chakula katika mazingira safi na salama, kuacha kula hovyo mitaani vyakula vilivyoandaliwa katika mazingira machafu na kuacha kutiririsha maji machafu hovyo mitaani.

“Mpaka leo Tunduma hatuna kesi ya Kipindupindu ambayo imeripotiwa lakini mwenzako akinyolewa wewe tia maji nywele zako, ni lazima tuchukue tahadhari mapema ili tuweze kuepuka ugonjwa huu” Amesema Mhe. Kihongosi.

Katika hatua nyingine DC Kihongosi amewahamasisha wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuwapeleka watoto shule hasa wale wa Awali, Darasa la Kwanza na Kidato cha Kwanza kwa kuwa tayari shule zimeshafunguliwa na masomo yameanza.

“Ndugu zangu wananchi nitoe wito, pelekeni watoto shule…hata kama hana sare wewe mpeleke, tutafanya utaratibu wa kupita shuleni kuangalia watoto ambao walipangiwa lakini mpaka sasa hawajaripoti na tutashuhulika na wazazi wao” Amesema Kihongosi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo amesisitiza kuwa michango ya hiari ambayo wazazi wakubaliana kwenye vikao vyao pamoja na uongozi wa shule kuhusu kuchangia chakula cha watoto wakiwa shuleni, isiwe chanzo cha baadhi ya watoto kufukuzwa ama kutopokelewa kuanza masomo shuleni kwa kuwa wazazi wao hawajachangia.

“Kwa kuzingatia muda mwingi ambao watoto wanautumia shuleni suala la chakula ni la muhimu hivyo, kupita Maafisa Maendeleo ya Jamii, Waheshimiwa Madiwani na Watendaji Kata na Mitaa tutaendelea kutoa elimu kwa wazazi kuchangia chakula hasa kipindi cha mavuno.” Amesema Chaurembo.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihingosi amefanya mkutano huoo maalum kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wafanyabiashara, Wajasiriamali na Wananchi kastika Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma kilichopo eneo la Mpemba.


Matukio katika Picha:

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi akizungumza na Wananchi, Wafanyabiashara na Wajasiriamali mbalimbali kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Ayubu Mlimba akizungumza na Wananchi, Wafanyabiashara na Wajasiriamali mbalimbali kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Momba ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi kwenye Mkutano wa kusikiliza kero zao uliofanyika kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma  wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Momba ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Wananchi wakiuliza maswali wakati wa Mkutano wa kusikiliza kero zao uliofanyika kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma  wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Momba ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Viongozi na baadhi ya Wataalam wakijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi kwenye Mkutano wa kusikiliza kero zao uliofanyika kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma  wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Momba ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa kusikiliza kero zao uliofanyika kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma  wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Momba ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi (katikati), baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Ayubu Mlimba wakiwasikiliza Wananchi, Wafanyabiashara na Wajasiriamali mbalimbali kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi tarehe 16 Januari 2024.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi akikagua miundombinu kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma mara baada ya kumaliza mkutano wa kusikiliza kero za Wananchi uliofanyika kituoni hapo tarehe 16 Januari 2024.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa