• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DC LULANDALA ALIONGOZA BARAZA LA MADIWANI LA TUNDUMA ZIARANI MOSHI

Imewekwa : March 2nd, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Fack Lulandala ameliongoza Baraza la madiwani na Baadhi ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo katika ziara ya siku Mbili Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro

Halmashauri ya Mji Tunduma imekuwa ikifanya vizuri sana katika ukusanyaji wa mapato na elimu kwa nia ya kufanya vizuri katika utunzaji wa Mazingira na Usafi baraza la madiwani likaona lifanye ziara ya siku mbili kwa ajili ya kujifunza mbinu nzuri wanazozitumia Manispaa ya Moshi katika zoezi zima la usafi

Akiongea wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Fack Lulandala amesema kuwa Halmashauri ya Mji Tunduma imefanya chaguo sahihi kabisa kwani Manispaa ya Moshi inang’aa mitaa yote na hakuna takataka barabarani wala katika mitaro

“Hongereni sana Manispaa ya Moshi kwa kazi nzuri mnayoifanya katika usafi, tangu nimeingia Moshi naona kila eneo ni safi sioni makopo wala takataka zozote barabarani na mitaani kwakweli mnafaa kuwa darasa la Halmashauri nyingine kuja kujifunza hapa” alisema Mhe. Lulandala

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Philemon Magesa ameeleza kuwa Tumejifunza Moshi kuwa jambo la usafi ni ajenda ya kudumu na ipo tangu zamani hivyo hapa kinachotakiwa ni elimu kwa watu wajue umuhimu wa kutunza mazingiza kwanza na hapo tutafanikiwa kuibadilisha Tunduma

“Tunaondoka na somo kubwa la kwenda kuibadilisha jamii ya Tunduma ili wajue swala la Usafi ni swala la maisha yetu ya kila siku hivyo lazima kila mtu afanye usafi bila kusukumwa na sheria za Halmashauri, jamii yetu tukiielimisha vya kutosha basi swala la Usafi Tunduma litakuwa la kudumu kama ilivyo Manispaa ya Moshi kwa sasa hadi tunakuja kujifunza” alisisitiza Mkurugenzi Magesa

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Mhe. Ayubu Mlimba amesema kutokana na nia ya Halmamashauri ya Mji wa Tunduma kuwa Manispaa lazima tujifunze kwa wakongwe wanaofanya vizuri ndio maana tumeamua kuja Moshi

“Jambo kubwa nililojifunza hapa kumbe hatutakiwi kuziogopa takataka maana ni Fursa kubwa sana na kuzichukia taka ni zambi kwani ni chanzo kikubwa sana cha mapato katika Halmashauri ni kujua tu kuzibadilisha na kuwa kitu kingine ambacho kinaweza kuwa Mbolea au mapambo inategemea na ubunifu wa Halmashauri Husika mlivyojipanga” alisema Mhe. Mlimba

Mhe. Mlimba ameyasema hayo alipotembelea Guba la Manispaa ya Moshi na Kukuta kiwanda cha kuzalisha Mbolea ya Asili (Mboji)

Katika kudhibiti uchafuzi wa Mazingira unaotokana na kelele, mitetemo, maji taka, hewa chafu na ardhi,  Halmashauri ya Manispaa ya Moshi  inafanya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali, Pia inatoa elimu kwa jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa mazingira na athari zake. Sheria za Mazingira pamoja na sheria ndogo za Halmashauri hutumika kudhibiti uchafuzi wa Mazingira.

 

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa