• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DC MBOZI AWAPA WANAWAKE SIRI YA MAFANIKIO, AWAPA USHAURI WATEULE WA RAIS

Imewekwa : March 9th, 2023

MBOZI. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amewataka wanawake wa mkoa wa Songwe kutokata tamaa wakati wanapoanguka katika safari ya kujikwamua kiuchumi bali wapambane huku akiwashauri wanawake walioteuliwa na Rais Samia Suluhu katika nafasi mbalimbali kufanya kazi kwa bidii.


DC Mahawe amesema hayo leo Jumatano Machi 8, 2023 akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dk Francis Michael wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yanafanyika katika viwanja vya CCM Vwawa wilayani Mbozi.


Amesema kuwa katika zama hizi mwanamke anatakiwa apambane na pale anapojaribu na kufeli asikate tamaa.


"Tukikaa tukisubiri kuwezeshwa tutachelewa, hizi ni kauli ambazo zimetucheleweshwa kwamba katika mafanikio ya mwanaume mwanamke yuko nyuma" amesema DC huyo na kuongeza;


Tumezubaishwa, sasa hivi ni pembeni ya kila baba aliyeendelea yuko mama na pembeni ya kila mama aliyeendelea kuna baba" amesema


Amesema sababu inayowachelewesha wanawake wengi ni kutokujiamini hivyo kutoa wito kwa wanawake wajiamini.


"Kutokujiamini na kutothubutu, mwanamke unaweza sana, ukianguka nyanyuka anza tena.. kufeli ni sehemu ya kukupeleka kwenye mafanikio, feli sana na jaribu sana utafanikiwa" amesisitiza


Ametoa wito kwa wanawake ambao wamepata nafasi hasa za kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassani katika ngazi mbalimbali kufanya kazi kwa bidii ili kudhihirisha kuwa wana uwezo.


"Niwaombe wanawake tulioaminiwa na Rais Samia tusijaribu kumuangusha, tunaweza sana tuamini kuwa tunaweza" ameshauri


"Ni neema Mungu kumchagua Rais Samia ili kuonyesha mfano kuwa wanawake tunaweza" amesisitiza

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewashauri wanawake waliopata nafasi kutowadharau waume zao.


"Nafasi ya mwanaume itabaki palepale, sio kuwa mwanamke umepata fursa ndio uwadharau wanaume hapana, hata kama una fedha kuliko yeye, Mungu akupe hekima

Sio una fedha zako nyumbani unataka uwe kiongozi" ameshauri DC huyo huku washiriki wakishangilia


"Tukipewa hizi nafasi zisiwe sehemu ya mateso kwa waume zetu" amesema

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa