• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DC MOMBA AWAKONGA NYOYO WAZEE WA TUNDUMA

Imewekwa : October 1st, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Fakii Lulandala ameshiriki siku ya maazimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika Ukumbi wa Honeymoon Hotel uliopo kata ya Makambini. Wakati anaongea na wazee hao Mhe. Fakii lulandala aliwaambia wazee kuwa

 “Mkinihitaji mimi muda wowote nitakuja kuwasikiliza, tena msiniombe mniambie mtotowetu njoo, mimi nitakuja kuwasikiliza na kutatua kero zenu” 


Serikali inatambua umuhimu wa wazee katika maendeleo ya taifa letu. Aidha serikali inatambua kuwa wazee ni hazina na rasilimali muhimu katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi yetu. Misingi ya nchi tuliyonayo sasa imejengwa na wazee wetu. Wazee ndio wamesaidia ukombozi wa nchi hii pamoja na ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika. Umoja wa Kitaifa tulionao, amani tunayojivunia, maliasili mbalimbali na utamaduni wa Mtanzania zimetokana na mchango wa wazee tulio nao katika taifa letu. Mchango uliotolewa na  wazee wetu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii ndio matokeo ya kuwepo kwa taifa letu.

 

Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema ‘‘Ustahimilivu na mchango wa wazee ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa’’. Kauli Mbiu hii inatukumbusha kuwa familia inawajibika kwa kiasi kikubwa katika kutoa huduma za msingi kwa wazee.

Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 inatoa maelekezo kuwa familia itaendelea kuwa taasisi ya msingi katika kutoa matunzo kwa wazee.  Katika makazi itakuwa kimbilio la mwisho baada ya njia nyingine za matunzo kushindikana.

Serikali imekuwa ikitoa huduma kwa wazee kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, Sera ya Afya 2007 na Miongozo mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha wazee wanastawi vyema na kupatiwa fursa sawa pasipo kubaguliwa kwa namna yeyote ile.

Wote tunafahamu Suala la uzee na kuzeeka limekuwa lenye umuhimu mkubwa kwa Taifa kwa ujumla hasa kuhusiana na mitazamo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Wazee ni moja ya kundi lililokuwa limetengwa katika jamii na hivyo nguvu za ziada kutoka kwa serikali na wadau kwa ujumla zimeendelea kufanyika ili kuhakikisha wanapatiwa haki zao za msingi.

“Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wazee msaidie juhudi za kulinda utamaduni na maadili mema ya Watanzania. Mmonyoko wa maadili umekithiri katika jamii” alisema Mhe. Fakii

Aidha, kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya Watoto. Ni vyema wazee wetu mkaendelea kutukumbusha tamaduni na maadili yatakayosaidia kuwa na jamii inayoheshimu utu, usawa wa kijinsia na yenye ari ya kushiriki shughuli za maendeleo.

Ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wazee; serikali itafanya yafuatayo;

  • Kutoa elimu kwa familia na jamii kuhusu wajibu wao katika kutunza wazee
  • Kuhimiza jamii kutoa matunzo kwa wazee wasio na ndugu
  • Kuendelea kuhimiza Utungaji wa Sheria ya Wazee
  • Aidha, serikali itahakikisha wazee wanashiriki na kushirikishwa katika masuala mbali mbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kuzingatia kanuni na sera za nchi

 

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa