• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Halmashauri Itaendelea Kubadilisha Mguu wa Ebeneza: Chaurembo

Imewekwa : August 14th, 2024

Na Benton Nollo, TTC 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariamu Chaurebo amesema baada ya Rais Samia Suuhu Hassan, Rias wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutimiza ahadi ya kumnunulia mguu wa bandia Ebeneza Mwakasyele (8) mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Shule ya Msingi Tunduma, Ofisi yake itahakikisha inabadilisha mguu huo kila muda utakapokuwa unahita mpaka mtoto huyo atakapotimiza miaka 18.

Chaurembo ameyasema hayo ofisini kwake tarehe 13 Agosti, 2024 baada ya Mwanafunzi huyo kupatiwa matibabu ya mguu bandia kufuatia ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia ofisi yake kugharamia matibabu ya Mguu wa Bandia kwa Mwanafunzi huyo baada ya kumuona akiwa miongoni mwa Wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wake uliofanyika Kata ya Uwanjani Tunduma mjini tarehe 18 Julai 2024, akiwa njiani kuelekea Mbeya akitokea mkoani Rukwa alikokuwa na ziara ya kikazi.  

“Ibeneza amepatiwa matibabu yote anayostahili na kama ambavyo Mheshimiwa Rais alivyoelekeza, kwa hivi sasa tuo tayari kumkabidhi shuleni ili aweze kuendelea na masomo yake…aidha, nimshukuru sana Rais wetu kwa moyo wake wa upendo wa kujali Wananchi wake na kuona ipo haja kumsaidia mtoto huyu, tunamuombea maisha marefu na Mwenyezi Mungu aweze kumbariki alichotoa na amuongezee zaidi.” Amesema Chaurembo na kuongeza;   

“Binafsi nimekubaliana na wenzangu (Menejimenti) kuwa ili azma ya Mheshimiwa Rais itimie kwa ukamilifu na uendelevu wake, nimeandika barua kwa Wakurugenzi wenzangu watakaofuata katika Halmashauri hii kutekeleza maelekezo ya kumnunulia mguu mtoto huyo pale itakaohitajika kwa kuwa anakua hivyo huenda kukawa na haja ya kufanya hivyo kwa kadiri madaktari watakavyoshauri.

Ebeneza alizaliwa tarehe 04 Septemba 2016 Mtaa wa Mwakakati Shina Moja katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe katika familia ya Mzee Mwakasyele, ambapo alizaliwa bila ulemavu wowote.

Ebeneza alikatwa mguu mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka minne (4) baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliosababisha mguu kuanza kuvimba, kutoa malengelenge na kufanya ngozi ya mguuni kuanza kukauka ambapo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi (Vwawa) ambako ilishauriwa apelekwe Hospitali ya Consolata iliyopo Ikonda mkoani Njombe na baada ya uchunguzi wa madaktari ilishauriwa akatwe mguu hali iliyomfanya kukosa amani hata aliokuwa akicheza na watoto wenzie.

Kwa upande wake Ebeneza amesema amepitia changamoto kubwa sana baada ya kukatwa mguu ikiwepo kushindwa kutembea licha ya kusaidiwa na wenzake alipohitaji msaada akiwa darasani, na wakati mwingine alihisi kunyanyapaliwa na jamii.

"Nilikuwa najisikia mpweke kutokana na hali ya kuwa tofauti na wenzangu lakini kaka yangu na wanafunzi wenzangu walikuwa wananisaidia sana pindi nilipokuwa nahitaji msaada." Amesema Ebeneza.

Hivyo, Ebeneza amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kumnunulia mguu wa bandia ambao amemuahidi kusoma kwa bidii ili atimize ndoto zake za kimaisha.

Naye Mama Mzazi wa Ebeneza, Atwanukiye Sanga amesema Ebeneza amepitia changamoto kubwa sana kabla na baada ya kukatwa mguu kwani alikosa malezi ya baba yake ambaye walitengana mwaka 2019 baada ya mtoto wao kuanza kuumwa bila kujua hatima ya ugonjwa huo.

 “Baada ya kukatwa mguu huo mwanangu alikuwa mpweke sana nilichukua jukumu la kumpeleka Shule ya Msingi Tunduma, Kitengo cha watu wenye mahitaji maalumu ambapo kila siku nilikuwa nampeleka shuleni na kumrudisha nyumbani ili atimize ndoto zake za kielimu kwa kuwa ni haki yake ya msingi.” Amesema Sanga.

Amesema kutokana na changamoto hiyo alipofika Darasa la Kwanza alimtafutia gongo la mti alilodumu nalo mpaka Darasa la Pili ambapo Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Mhe. David Silinde alimnunulia gongo la chuma alilolitumia mpaka Rais Samia alipotoa msaada wa kumnunulia mguu wa bandia.

“Namshukuru sana Rais Samia kwa msaada wa kumnunulia mguu wa bandia mwanangu hali ambayo itamsaidia kuhudhuria masomo na kutimiza ndoto zake kimaisha kwani Ebeneza anatamani sana kuwa daktari bingwa,” Ameongeza Sanga.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tunduma, Suzana Mwakibete amesema Ebeneza alianza shule Darasa la Awali mwaka 2021 Kitengo cha Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu ambao walikuwa 104, ambapo uhitaji wake ulikuwa mkubwa sana ukilinganisha na wenzake shuleni hapo kwani alikuwa anatambaa muda wote.

“Tunatarajia baada ya Ebeneza kupatiwa mguu ataondokana na changamoto ya kutembelea mguu mmoja na kuhudhuria masomo kikamilifu.” Amesema Mwakibete.

Matukio katika Picha:

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo (aliyevaa miwani) akiwa katika picha ya pamoja na Mwanafunzi Ebeneza Mwakasyele (wa pili kushoto) baada ya kupatiwa matibabu ya Mguu wa Bandia. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Shughuli za Lishe Halmashauri ya Mji Tunduma, Dkt. Sebastian Siwale, wa kwanza kushoto ni Mama Mzazi wa Ebeneza, Atwanukiye Sanga.

Mwanafunzi Ebeneza Mwakasyele kabla ya kupatiwa matibabu ya Mguu wa Bandia. (Picha zote na Julius Evandino).

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa