• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA TUNDUMA

Imewekwa : January 20th, 2023

Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefunga safari na kuja katika Halmashauri ya Mji Tunduma lengo ni kujifunza jinsi ya kubuni vyanzo vya mapato na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 20/01/2023 kwa kutembelea baadhi ya vyanzo vya mapato na miradi ya maendeleo ikihusisha Madiwani 41, Wataalamu 9 na Madereva 2

Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe. Ibrahimu Issa Chiputula amesema kuwa Baada ya kuona Halmashauri ya Mji Tunduma inafanya vizuri katika ukusanyaji mapato ndio maana Baraza la madiwani likaamua kuja kujifunza hapa Tunduma

 

“Tunawashukuru sana Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kutupokea na kukubali kutuelekeza mbinu mnazotumia katika kubuni vyanzo vya mapato na kukusanya mapato Hongereni sana, huu ndio uzalendo wa kweli katika nchi yetu” alisema Mhe. Chiputula

Mhe. Chiputula aliendelea kueleza kuwa wao Wilaya ya Masasi wanatarajia kuanzisha shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza na Mwanga sasa wameupata na wanaenda kuufanyia kazi ili waweze kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Mhe. Ayubu Itlan Mlimba aliwapongeza sana Madiwani na Wataalamu wa Wilaya ya Masasi kwa kuchagua kuja Tunduma kujifunza kwani Halmashauri zipo nyingi sana lakini wakaona wafike Tunduma

“Tunduma sasa tupo katika mchakato wa kuifanya kuwa Manispaa kwani vigezo vingi tumevifikia, nahii inasababishwa na ushirikiano wa dhati baina ya wataalamu na Baraza la madiwani katika kubuni vyanzo vya mapato na kukusanya mapato” alisema Mhe. Mlimba

Aidha mwenyekiti Mlimba alendelea kusema kuwa “Tunduma suala la mapato ni kipaumbele cha kwanza na wote tunaimba wimbo mmoja katika hili, ikitokea mwananchi amekiuka maadili ya ulipaji mapato wote tunaungana kumuelimisha na kumfanya atoe  tozo hizo na si kumkingia kifua asitoe” alisisitiza Mhe. Mlimba

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya Mhe. Salumu Kiyambi aliwaelekeza Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kuwa kutokana na usimamizi mzuri wa makusanyo sasa Tunduma inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani

“Sasa tunajenga miradi mikubwa mingi kwa mapato ya ndani mfano mmeiona Shule ya Msingi ya Ghorofa inayoitwa Haisoja iliyogharimu Milioni 829 yenye Madarasa 10, Ofisi 04 na Matundu ya vyoo 24 na Kituo cha Afya Chapwa chenye majengo nane (OPD, Maabara, Upasuaji, Mama na Mtoto, kufulia, Mochwari, kichomea taka na Nyumba ya mtumishi) kwa gharama ya milioni 640 tunajenga yote kwa kutumia mapato ya Ndani” alisema Mhe. Kiyambi

Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamefanya ziara ya siku moja ndani ya Mji wa Tunduma kwa kutembea Mpaka wa Tanzania na Zambia na kuona jinsi biashara za ujirani mwema zinavyofanyika kwa kutembelea Zambia na kuongea na baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wa Nchini Zambia


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa