• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

Imewekwa : May 25th, 2025

Na Benton Nollo, TTC

Timu ya Halmashauri ya Mji Tunduma wilayani Momba inayokwenda kwenye mashindano ya  Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) imeondoka leo tarehe 25 Mei 2025 kwenda wilayani Momba kwa ajili kushiriki mashindano hayo kwa ngazi ya Mkoa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, muda mfupi kabla ya timu hiyo kuondoka, Afisa Elimu ya Awali na Msingi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya UMITASHUMTA ngazi ya Halmashauri, Casta Mbawala amesema Timu hiyo inaondoka ikiwa na jumla ya Wanafunzi 120 wanaokwenda kushiriki michezo mbalimbali pamoja na Walimu wao 12.

Mbawala amesema Timu hiyo inaondoka kwenda kushiriki michezo ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe, baada ya kukaa kambini katika Shule ya Msingi Katete kujinoa kwa muda wa siku 5 ambapo Wanafunzi wamejiandaa vya kutosha na wana matarajio ya kupata makombe na zawadi kwa kushinda michezo hiyo.

"Michezo tunayokwenda kushindana ni mpira wa miguu kwa Wavulana na Wasichana, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono, Basket Ball (Mpira wa Kikapu)...kizazi kipya lakini pia Fani za ndani ambapo kuna Kwaya na Ngoma, michezo yote hiyo imeandaliwa vizuri." Amesema Mbawala na kuongeza;

"Watoto hawa tumeshawaandaa vizuri, Walimu wako imara tayari kwa michezo yao na tutakuwa kule kwa siku 4 kuanzia tarehe 26 hadi 29 Mei 2025 kwa mashindano ya Mkoa wetu wa Songwe ambayo yatafanyika katika Shule ya Sekondari Songwe Sunrise iliyopo wilayani Mbozi."

Aidha, Mbawala ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo kwa kuwezesha maandalizi mazuri ya vifaa pamoja na Walimu kwani kabla ya kuanza kambi, awali yalianza mashindano ya Kanda ambayo ndiyo yaliyotumika kuandaa Timu hiyo ya Halmashauri bila changamoto yoyote.

Kadhalika, Mbawala amewashukuru wadau na taasisi mbalimbali ambazo zimeshiriki kuchangia michango ya hali na mali kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.

Mashindano ya UMITASHUMTA yalianzishwa rasmi na Serikali mwaka 1971 hadi mwaka 2000 yaliposimamishwa ili kuyaboresha na baadaye mwaka 2007 yalirejea tena mpaka sasa licha ya kuwa mwaka 2019 yariahirishwa kwa sababu ya mlipuko wa UVIKO 19.

Matukio katika Picha:

(Picha zote na Benton Nollo, TTC).





Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa