• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

HITILAFU YA UMEME CHANZO CHA AJALI YA MOTO SOKO LA* *MANZESE, RC MGUMBA AMEIAGIZA TANESCO KUPITIA MFUMO WA MASOKO YOT.*

Imewekwa : November 27th, 2021



*TUNDUMA:* Hitilafu ya Umeme chanzo chanzo cha ajali ya moto uliotokea Novemba 16, katika Soko la Manzese na kupelekea Maduka 46 kuteketea kwa moto.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesoma taarifa ya Timu aliyounda mbele ya wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma ambao waliathirika na moto.


Akisoma taarifa ya uchunguzi Mkuu wa Mkoa amesema Timu imegundua wateja waliounganishiwa Umeme na TANESCO wamekiukwa mkataba kama vile kujiunganishia Umeme kiholela wateja 13 tu ndio walikuwa na mkataba na wengine walijiunganishia kiholela.


Wateja wametumia nyaya tofauti mfano wametumia 2.5mm badala ya waya za 4 hadi 6mm katika sehemu za swichi soketi, nyaya za taa zimepelekwa kwa maeneo yanayotumia Umeme mkubwa.


Wateja kuchanganya kiholela mifumo ya umeme kati ya wa nguvu za jua (Solar) na wa TANESCO bila kufuata taratibu sahihi za kutumia mifumo hiyo 2 na pale mfumo moja kutozimwa pale unapotumika mwingine.


Kuunganisha vifaa vingi vya umeme sehemu moja bila kuzingatia mahitaji na uwezo wa vifaa vinavyotumika, mfano wateja 4 walibainika kujiunganishia Umeme kupitia mita 1 na waliunga zaidi ya taa 55 zenye ukubwa Wati 20 kila moja ambapo matumizi ya nyaya hayakuzingatiwa.


"Hata hivyo baada ya timu kufanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara imegundulika kuliwai kutokea  Hitilafu kama hii lakini ulidhibitiwa mapema na TANESCO na Jeshi la Zimamoto" Omary Mgumba.


SABABU ZA MOTO KUSAMBAA

Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Timu imebaini moto ulisambaa kwa haraka kwa sababu zifuatazo.


Bidhaa nyingi zilizokuwepo sokoni ni nguo ambazo ni rahisi kushika moto kwa haraka


Ujenzi wa Nyumba ulikuwa na matumizi ya vitu ambavyo ni rahisi kushika moto kwa haraka, mfano PCV na NK.


Matumizi ya Gebo za majengo hayakuzingatia ili kutenganisha Kuta kwa mpangilio mzuri.


Hazikufanyika Jitihada za mapema na za haraka kufikisha taarifa ya moto kwa Mamlaka zinazohusika.


Kukosekana kwa gari la Zimamoto katika eneo la tukio, gari ya Tunduma ilikuwa kwenye matengenezo Mbeya.


Kushikamana kwa mapaa ya Nyumba


ATHARI ILIYOPATIKANA NA AJALI YA MOTO

Timu imebaini athari iliyobainika ni kuwa Jengo lililoungua halipaswi kukarabatiwa kwa kuwa limearibika sana kinachotakiwa ni kujenga upya.


Thmani ya jengo ni Milioni 123 ukiondoa Ardhi kwa kuwa Ardhi bado ipo na bidhaa zilizoteketea zinakadiriwa za  Milioni 475 na kufanya jumla Kuu Milioni 598.

HATUA AMBAZO SERIKALI INACHUKUA KUEPUSHA MAJANGA.


Barabara zote zilizofungwa zifubguliwe ndani ya mwezi moja, wale waliojenga kwenye Barabara wabomoe kwa gharama zao na hiari yao ikija kobomoa Serikali watalipa gharama izo za ubomoaji.


Halmashauri ya Mji wa Tunduma ipange aina moja ya Biashara katika sehemu moja na sio kuchanganya


Kuepo na Timu ya pamoja ya ukaguzi wa Nyumba za Makazi na Biashara ili kuepuka kujenga Nyumba sehemu ambayo sio sahihi.


TANESCO wapitie upya mfumo wote wa Umeme katika Soko la Manzese


Mapaa yaliyounganishwa na Nyumba zilizounganishwa zitenganishwe kwani Nyumba na Nyumba lazima uache uchochoro na wote waliojenga kwenye uchochoro wabomoe vibanda vyao.


Halmashauri ya Mji wa Tunduma na Jeshi la Zimamoto pamoja na Mamlaka nyingine wajenge visima vya Maji katika masoko na mikusanyiko ili majanga yanapotokea basi maji yanakuwepo.


Serikali kuongeza gari kubwa la Zimamoto hapa Tunduma kwa kuwa Mji wa Tunduma unakuwa sana kibiashara.


Viongozi wa masoko waache mara Moja tabia ya kuajili walinzi ambao hawajapitia mafunzo yoyote ya ulinzi kama vile Mgambo au JKT.


Pia Kampuni zinazopewa kazi za kulinda masoko lazima ziwe zinafuata kanuni, taratibu, sheria na mikataba waliyoingia na vyombo vyetu vya Usalama.


Wafanyabiashara wanakumbushwa kuzima vifaa vyote vya umeme pale wanapokuwa wanafunga ofisi zao kwa kuwa inahisiwa kuwa moto ulianza kwenye chumba cha kuuza simu na kunawezekano vifaa viliachwa bila kuzimwa


Serikali iendelee kuondoa vyumba vilivyoingia kwenye Barabara ya MIAMI Ili iweze kupitika kutoka sehemu moja kwenda nyingine


TANESCO itoe elimu kwa wafanyabiashara wote wa masoko ili waweze kupata ufahamu na uelewa pale majanga yanapotokea


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa