• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

IMBEJU KUWANUFAISHA VIJANA NA WANAWAKE TUNDUMA

Imewekwa : July 1st, 2023

Na William Maganga - Tunduma TC

Benki ya CRDB imekuja na mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake wa Tunduma ili kuwawezesha kiuchumi. Mkakati huo umezinduliwa leo katika ukumbi wa Tunduma sekondari TC huku mgeni rasmi akiwa katibu tawala wilaya ya Momba Bw. Frank Kinda, huku wahusika wakiwa ni vijana na wanawake. Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja wa benki ya CRDB tawi la Tunduma Bw. Chrispin Kombo, amesema mkakati huo wameupa jina la” IMBEJU”, ikiwa na maana ya uvumbuzi na mbegu (maendeleo).

Aidha meneja huyo ameyataja makundi yatakayonufaika na mtaji wezeshi kuwa ni wafanyabiashara ya Samaki, machinga, vikundi vinginevyo, fursa online n.k.  Ameongeza kuwa mfumo huo umetengenezwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki. Pia ametaja kuwa kiasi cha mtaji wezeshi unaanzia kiasi cha shilingi laki mbili (200,000) hadi Milioni Thelathini (30,000,000).

Katika uzinduzi huo Afisa maendeleo  wa mji wa Tunduma Bi.Mwanaisham Shemagembe   amesema katika 100% ya maendeleo ya Tunduma, kundi la wanawake limechangia 10%. Hivyo katika makusanyo ya mapato ya tunduma 2022/2023 yalofikia fedha za kitanzania billion 13. 10% ya fedha hizo zinarudishwa kwa wananchi, huku 4% kwa wanawake,4% kwa vijana na 2% kwa walemavu.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi Bw.Kinda ameipongeza sana benki ya CRDB kwa kuja na mtaji wezeshi (imbeju) wenye lengo la kukuza uchumi na kipato kwa watanzania. Katika mkakati huo pia ametaja manufaa kwa walengwa kuwa ni Pamoja na kuwezeshwa akaunti maalumu ya imbeju Pamoja na bima ya Maisha.

Akitoa ufafanuzi Zaidi kwa walengwa wa mtaji wezeshi, afisa mahusiano wa benki ya CRDB, amesema waombaji ni wale waliopo kwenye vikundi vilivyosajiliwa. Pia ameelezea kuwa namna ya upatikanaji wa mtaji wezeshi kwa wanawake ni kupitia vikundi vyao na kwa vijana utafanyika kwa njia ya mtandao (online application).

Ameongeza pia kwa kutaja sifa ya kijana anayestahili mkopo huo sharti awe ni mtanzania, awe na umri kati ya miaka 18-40, awe tayari ameanzisha biashara iliyo halali na awe amefaulu mtihani wa uombaji wa mtandaoni(ICTC). Kwa upande wa upande wa wanawake sifa zao ni miaka 18-60, awe mwanachama wa kikundi kilichosajiliwa na biashara iwe halali pia inafanyika Tanzania.

Katika sharti la biashara ya kufanyika Tanzania Bi.Sarah Laurent aliuliza swali kuwa je,imbeju itamsaidiaje mtu anayefanyia biashara zake upande wa Zambia?. Afisa mikopo amemjibu kuwa kwa vile ni mtanzania na kikundi chake kipo Tanzania na amekopa Tanzania hivyo ana sifa ya kupata mkopo.

Katika hafla hiyo afisa mikopo Bw. Fedrick Mwasi amefafanua juu ya bima kwa wanufaika wa mkopo huo kuwa wanashikwa mkono katika biashara, ajali,ulemavu na kifo, ambapo mhusika akifariki mkono wa pole ni kati shilingi Million moja na nusu  hadi million kumi (1,000,000-10,000,000), akifiwa na mwenza ni kati ya millioni moja hadi millioni tatu (1,000,000-3,000,000)

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa