• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

IRDO Yazindua Mpango wa Miaka Mitano

Imewekwa : March 12th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Farida Mgomi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe amezindua Mpango Mkakati wa Uhamasishaji wa Rasilimali wa Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini – IRDO kwa kipindi cha miaka mitano (2024/2028).

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa High Class mjini Tunduma tarehe 12 Machi 2024 na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo na wadau mbalimbali, Mgomi amelipongeza Shirika hilo kwa uthubutu huo wa kuonesha ushirikiano mkubwa na Serikali katika utekelezaji ya miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Mhe. Mgomi ameahidikuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo na mashirika mengineili kukamilisha afua zote kwa jamii zilizoainishwa katika mpango mkakati huo.

“Niwapongeze sana Shirika hili la IRDO kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya katika jamii yetu…kwani kupitia miradi yenu mnaikomboa jamii na mambo mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa chakula na lishe, kupinga ukatili wa kijinsia, kutoa elimu ya kupambana na virusi vya UKIMWI na kuwasaidia kupima na kuwaonesha mahali pa kweli baada ya kubainika kuwa wana Virusi vya UKIMWI…miradi ya vijana wa kike na wakiume waliobarehe kwa kuwapatia elimu mbalimbali…kwa kweli makundi yote haya yanahitaji kusaidiwa.” Amesema Mhe. Mgomi na kuongeza;

“Shirika hili limetoa fursa kwa vijana hawa wa kike na kiume ili waweze kujitambua na kujitunza na kufikia ndoto zao salama…hamkuishia hapo pia, mnashughulika na kuwasaidia vijana wetu walioathirika na madawa ya kulevya kwa kuwapatia dawa kupitia Kituo chetu cha Afya cha Tunduma…hii ni kazi kubwa na mnastahili pongezi.”

Awali akiwasilisha  vipaumbele vya IRDO, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dr. Simon Chiwanga ameeleza kuwa lengo kubwa la Shirika ni kuinua maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia miradi ya kilimo endelevu, elimu ya ujasiriamali na masoko, uhakika wa chakula, uboreshaji lishe, afya ya jamii kwa maana ya kutokomeza maambukizi mapya ya VVU na afya ya uzazi.

Chiwanga ametaja malengo mengine ya Shiriki kuwa ni upatikanaji wa maji safi na salama, kutokomeza ukatili wa kijinsia na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuboresha mazingira, na kuwa na timu yenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa kutekeleza shughuli zote katika mpango huo.

 Shirika la IRDO lilianzishwa mwaka 1989 kwa lengo la kuziwezesha jamii zilizosahaulika kwa kushirikiana na AZAKI na wadau wengine kwa kutambua rasilimali zao na kuziboresha kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kuendeleza mifumo ya maisha bora nchini Tanzania.

Matukio katika Picha:



Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mei Mosi Songwe Yafana

    May 01, 2025
  • Chaurembo Awapongeza Walimu

    April 30, 2025
  • Tunduma kwa Taaluma Sina Mashaka Nanyi: RAS Seneda

    April 30, 2025
  • Chaurembo Afungua Mafunzo Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili

    April 29, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa