Halmashauri ya Mji Tunduma inatekeleza mradi wa Ujenzi wa jengo la Utawala lenye thamani ya shilingi Billion tatu na milioni mia moja (TZS 3,100,000,000/=) katika Kata ya Chapwa Mtaa wa Msampania. Mradi huu utatekelezwa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza ilianza mwaka wa fedha wa 2020/2021 na utekelezaji ulianza tarehe 12 April 2021 baada ya kupokea fedha za awamu ya kwanza na sasa ni awamu ya pili iliyoanza 26 February 2022 baada ya kupokea fedha za awamu ya pili.
Mpaka kufikia leo 22/03/2022 Halmashauri ya Mji Tunduma imepokea jumla ya fedha kiasi cha shilingi 1,750,000,000 katika ujenzi huu
Halmashauri ya Mji Tunduma iliingia Mkataba kwa awamu ya pili na Mkadiriaji majenzi Boaz Y. Kagobe wa S.L.P 3541 Mbeya kwa mfumo wa manunuzi wa Labour based contract wenye jumla ya shilingi 63,000,000/= ambayo inajumuisha umaliziaji wa jengo kwa upande wa chini kwa kazi zote ili lianze kutumika “ground floor”, umaliziaji wa nguzo za juu, beam na kupaua “first floor”.
Katika mkataba huu wa awamu ya pili kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kama zifuatazo:-
Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kama zifutazo:-
Mradi huu ukikamilika utakuwa mkombozi kwa wakazi wa Mji wa Tunduma pamoja na Halmashauri ya Mji wa Tunduma kwa sababu utawezesha kuepusha gharama ya kukodi jengo la Ofisi kwa Tshs. 40,000,000.00 (Milioni Arobaini) kwa mwaka.
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa