• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Kamati ya Siasa CCM Mkoani Songwe Yaridhishwa, Utekelezaji Miradi Tunduma

Imewekwa : January 25th, 2024

Kamati ya Siasa CCM Songwe Yaridhishwa, Utekelezaji Miradi Tunduma

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe tarehe 25 Januari 2024 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Tunduma ambapo imeridhika na utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Radwel Mwampashi amesema Kamati hiyo imeridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati.

Mwampashi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega na bega na Wananchi wake na kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi katika Halmashauri ya Mji Tunduma, hii inaonesha wazi kuwa Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa amedhamirtia kwa dhati kuwaletea maendeleo Wananchi wake…hakika Serikali inaonekana kupitia miradi hii” Amesema Mwampashi.

Pia, Mwampashi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Wilaya ya Momba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kufuatilia na kukagua miradi hiyo mara kwa mara  hali inayofanya miradi hiyo kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Aidha, Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema pamoja na kufurahishwa na utekelezaji wa miradi, wametoa rai na kuwaasa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kuwa wazalendo katika kutekeleza wajibu na majukumu yao ili kuweza kukamilisha mipango ya maendeleo ambayo Halmashauri inajiwekea.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo amewahimiza watumiaji wote wa miundombinu hiyo kuhakikisha kuwa inatunzwa kwani Serikali inatumia fedha nyingi kuboresha na kutatua changamoto ambazo zinaikabili jamii ili iwe na manufaa kwao na kizaji kijacho.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael ameiarifu Kamati hiyo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeupatia Mkoa wa Songwe fedha Zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa ajili ya kutatua kero ya uhaba wa maji safi na salama kwa wananchi wake ambapo amewataka Waheshimiwa Madiwani kutumia majukwaa yao kuwatoa hofu wananchi kuhusu tatizo la ukosefu wa maji safi katika maeneo yao.

“Waheshimiwa Madiwani ni lazima mfahamu kwa undani mipango ya Serikali katika kupambana na changamoto zinazowakabili Wananchi wake na jitihada hizo mziseme kwa Wananchi ili muwatoe hofu na wawe na imani na Serikali yao.” Amesema Dkt. Michael na kuongeza;

“Waheshimiwa Madiwani ninyi ndiyo wa kuisemea Serikali kwenye majukwaa yenu ya kisiasa, hivi karibuni mkoa wetu tumepokea fedha zaidi ya shilingi milioni 70 ambazo zitatoa maji Mto Momba kuja katika Mji wa Tunduma, Mlowo na Vwawa…mradi huu ni mkubwa na unakuja kumaliza adha ya maji katika Mkoa wetu wote wa Songwe na tayari Wizara ya Maji ipo kwenye hatua za kumpata Mkandarasi ili utekelezaji uanze.”  

Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ina thamani ya shilingi bilioni 8.2 ambayo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia SH (ambapo zinatumika shilingi bilioni 5.1), Ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Mwakakati (hapa zinatumika shilingi milioni 702.4), Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Chipaka (napo zinatumika shilingi milioni 583).

Miradi mingine iliyotembelewa na kukaguliwa ni ujenzi wa madarasa kumi (10) ya Ghorofa, nyumba ya Walimu mbili kwa moja (2 in 1) Shule ya Sekondari Uwanjani (zinatumika shilingi bilioni 1.1) na Mradi wa Usambazaji Maji wa Mwalimu Nyerere ambao mpaka kukamilika kwake utagharimu shilingi milioni 702.4.


Matukio katika Picha:

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe, Radwel Mwampashi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Dkt. Samia SH akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 25 Januari 2024.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe tarehe 25 Januari 2024 imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Dkt. Samia SH iliyopo Mtaa wa Namole, Kata ya Chiwezi ambapo mpaka sasa zinatumika shilingi bilioni 5.1.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Francis Michael (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Dkt. Samia SH iliyopo Mtaa wa Namole, Kata ya Chiwezi tarehe 25 Januari 2024 ambapo mpaka sasa zinatumika shilingi bilioni 5.1.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo (aliyevaa kilemba cha bluu) akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Dkt. Samia SH iliyopo Mtaa wa Namole, Kata ya Chiwezi tarehe 25 Januari 2024 ambapo mpaka sasa zinatumika shilingi bilioni 5.1.

Diwani wa Kata ya Chiwezi, Mhe. Frances Sikanyika akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Dkt. Samia SH iliyopo Mtaa wa Namole, Kata ya Chiwezi tarehe 25 Januari 2024 ambapo mpaka sasa zinatumika shilingi bilioni 5.1.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi (kulia) akimsikiliza kwa makini Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS Mkoa wa Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga (kushoto) walipokuwa wakizungumza, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Dkt. Samia SH iliyopo Mtaa wa Namole, Kata ya Chiwezi tarehe 25 Januari 2024 ambapo mpaka sasa zinatumika shilingi bilioni 5.1.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dkt. Samia SH, Anna Salutary Mushi akitoa taarifa ya shule wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Dkt. Samia SH iliyopo Mtaa wa Namole, Kata ya Chiwezi tarehe 25 Januari 2024 ambapo mpaka sasa zinatumika shilingi bilioni 5.1.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe tarehe 25 Januari 2024 imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Mwakakati  katika Kata ya Mwakakati.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe tarehe 25 Januari 2024 imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Chipaka katika Kata ya Chipaka ambayo inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 583 kupitia SEQUIP.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe tarahe 25 Januari 2024 imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji Uhuru Mwl. Nyerere unaotekelezwa katika Mitaa ya Majengo Mapya, Mwl. Nyerere na Msongwa ambao unatekelezwa kwa Force Account kwa gharama ya shilingi milioni 605.2 ambapo mpaka sasa Serikali kupitia Mfuko wa Maji wa Taifa - NWF imeshaleta shilingi milioni 400 kati ya shilingi milioni 702.4.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe tarehe 25 Januari 22024 imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi (10) ya Ghorofa, nyumba ya Walimu mbili kwa moja (2 in 1) Shule ya Sekondari Uwanjani (zinatumika shilingi bilioni 1.1). (Picha zote na Benton Nollo).


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa