• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Kikao cha Huduma za Lishe Chafanyika

Imewekwa : May 21st, 2025

Na Benton Nollo, TTC

Kamati ya Huduma za Lishe katika Halmashauri ya Mji Tunduma imefanya kikao chake cha kawaida kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 21 Mei 2025.

Pamoja na mambo mengine, Kamati hiyo imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Afua za Lishe katika kipindi hicho kwa Kitengo cha Huduma za Lishe, Divisheni ya Elimu Msingi na Awali, Diivisheni ya Elimu Sekondari, Divisheni ya Maendeleo ya Jamii na Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kuhusu matibabu ya  utapiamlo mkali, jumla ya watoto 13 wametibiwa katika kipindi hicho ambapo kwa upande wa huduma ya elimu ya namna nzuri ya kuimarisha lishe wakati wa ujauzito, unyonyeshaji na ulishaji watoto wachanga na wadogo imekuwa ukitolewa kila siku maeneo ya kliniki ya huduma za afya ya uzazi na mtoto ambapo watoto wachanga 7,716 wamepatiwa maziwa ya mama pekee ndani ya miezi 6.

Aidha watoto 32,409 walichukuliwa hali za lishe na walezi kupatiwa unasihi wa lishe ambapo baada ya uchunguzi, watoto 999 walikuwa na uzito pungufu kiasi na watoto 423 walikuwa na uzito pungufu sana, watoto 277 walikuwa na ukondefu kiasi na watoto 234 walikuwa na ukondefu sana.

Kuhusu utoaji wa vidonge vya madini chuma, katika kipindi hicho kati ya Wajawazito 11,483, Wajawazito 11,062 walihudhuria kliniki na kupatiwa vidonge hivyo ambapo walizaliwa watoto 2,368 na kati yao watoto 229 walikuwa na uzito wa chini ya kilo 2.5.

Kadhalika, kuhusu utoaji wa Matone ya Vitamini A na Dawa za Minyoo katika kipindi hicho watoto 11,410 wamepatiwa Vitamini A na watoto 3,475 wamepatiwa vitonge vya minyoo.

Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe kwenye Mitaa, yamefanyika kwa Kata zote 15 na Mitaa yote 71 ambapo walezi 4,307 wenye watoto wenye umri wa miezi 0 - 23 walipatiwa unasihi, watoto 7,583 walipimwa mzunguko wa mkono - MUAC ambapo kati yao watoto 75 walikuwa na utapiamlo wa kadiri na watoto 2 walikuwa na utapiamlo mkali na walipatiwa rufaa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ya matibabu ya utapiamlo mkali.

Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa