• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

KIKAO KAZI CHENYE TIJA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA

Imewekwa : May 18th, 2022

Tunduma: watendaji wa kata na mitaa ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma wamehudhuria kikao kazi cha siku moja ambacho kililenga kuwajengea uwezo na kuwawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku

Akiongea katika kikao kazi hicho Mkuu wa Divisheni ya Utawala na  Usimamizi wa Rasilimali watu Ndugu Josephat Kayombo amewakumbusha watendaji wa kata na Mitaa kutimiza wajibu wao katika kusimami kata na mitaa na kuonyesha mfano wa kuigwa katika kusimamia miradi ya maendeleo


“Kila Mtendaji ahakikishe anashiriki kikamilifu katika kuibua, kusimamia na kushiriki katika miradi ya maendeleo inayoendelea katika Mtaa wa kata husika, sitegemei kuona viongozi toka Halmashauri kuja kuhamasisha Wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo wakati Mtendaji wa Mtaa na kata husika upo”


Pia Bwana Kayombo aliwakumbusha kila Mtendaji wa Mtaa na Kata ahakikishe anaitisha vikao na kusoma Mapato na matumizi kwa wananchi ili waendelee kujua Michango wanayotoa inafanya kazi gani.

Pia miradi yoyote inayopelekwa na Serikali kuu au za mapato ya ndani wananchi wanatakiwa kuambiwa ili waijue na wajue kuwa inaletwa katika kuwasaidia mahitaji yao kwani miradi hiyo inatekelezwa kutokana na kodi wanazozitoa.


Naye Bwana Bakari Ibrahimu Kaimu Mkuu wa Idara ya Usafi na Usimamizi wa Taka, Katika suala la kusimamia Usafi amewakumbusha watendaji wa Mitaa na kata wote kuwa ni jukumu la kila mtu kuhakikisha mtaa wake na kata kwa ujumla iko safi. Wasimamie zoezi zima la uzoaji wa taka katika mitaa yao.

“Kila mtendaji wa mtaa anawajibika kuhakikisha mtaa wake unakuwa msafi kwa kuhamasisha wananchi kutunza taka na kuzitoa siku ya ratiba ya gari la taka kupita katika mtaa husika, wananchi wanapotupa taka barabarani au mitaani hovyo maana yake mtendaji wa mtaa husika hujatimiza wajibu wako”

Kwa upande wake Afisa Mapato wa Halmashauri ya Mji Bi. Dora Mbembela amewakumbusha watendaji kusimamia mapato katika kata na mitaa yao kwani kumekuwa na biashara nyingi ambazo zinaanzishwa huko mitaani au mapato mengi yanapita katika mitaa hivyo wanatakiwa kuhakikisha wanawazuia wote wanao torosha mapato.


“Ikumbukwe tumewapatia Mashine za Kutoza Ushuru (POS) ili mzitumie na mapato yake yaingie Benki kila siku”


Bi Dora aliendelea kusema kuwa kila mtendaji mwenye POS ahakikishe halali na pesa nyumbani badala yake pesa ipelekwe Benki na kuingizwa katika akaunti ya Halmashauri.

“Unapolala na pesa sheria hairuhusu, pia ulinzi wa pesa unakuwa mdogo au unaweza kushawishika kuzitumia na mwisho wa siku ukajikuta unapata matatizo kwa kuchukulia hatua za kisheria kwani unakuwa umekiuka misingi na taratibu, hivyo nawakumbusha sana kupeleka pesa benki”


Naye Afisa Utumishi na rasilimali watu Bwana Raphael Simkonda aliwakumbusha wajibu na majukumu wa watendaji wote katika utekelezaji wa kazi za kila siku.

Bwana Simkonda aliwaambia kuwa vibali vya ujenzi sasa vinagatuliwa kuja kwenu hivyo kuna utaratibu utaletwa wa kuunda kamati ili muweze kutekeleza jukumu hilo kwani wananchi ni wengi sana wanaoanza kujenga nyumba hivyo vibali vikitolewa huko itakuwa ahueni sana katika kuwapunguzia adha wanachi kuja Halmashauri

Pia aliwakumbusha kusimamia lishe katika mitaa yao.


“Katika kila vikao vyenu waelekezeni wananchi kuhusu lishe bora husani kwa watoto ili tuondokane na Utapiamlo pamoja na Udumavu wa watoto, ikumbukwe kuwa lishe bora ni vyakula tulivyonavyo majumbani sasa ni jinsi gani wavitumie ndio wengi hawajui hivyo nendeni mkawalekeze”


Mwisho Bwana Simkonda aliwakumbusha kuwa kila mmoja anatakiwa kuwa na mpango kazi wa wiki na anatakiwa kuusimamia ili kuleta matokeo chanya katika majukumu ya kila siku

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa