• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Kikwete: Tunduma Mmetekeleza Maagizo ya Rais Samia

Imewekwa : February 25th, 2025

Na Benton Nollo, Tunduma TC

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) amesema Halmashauri ya Mji Tunduma imetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 kwa vikundi 150 vya Wanawake Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Waziri Kikwete ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua Kikundi cha Vijana cha Ufugaji Kuku na Uuzaji wa Mayai cha Chipaka wakati wa ziara yake ya siku moja Halmashauri ya Mji Tunduma wilayani Momba aliyoifanya tarehe 25 Februari 2025.

Mhe. Kikwete amebainisha kuwa katika kuhakikisha mikopo hiyo inakuwa na tija kwa Walengwa, Mhe. Rais Samia alielekeza kusitisha utoaji wa mikopo hiyo na badala yake aliagiza mamlaka husika kupitia upya na kufanya maboresho ambapo baada ya mchakata huo kukamilika, dirisha la utoaji mikopo lilifunguliwa rasmi mwezi Septemba 2024.

"Mheshimiwa Rais Samia amezielekeza Halmashauri zote nchini kuanza kutoa mikopo hiyo kwa kutumia mfumo mpya wa utoaji na usimamizi wa mikopo hiyo na ninyi mmetekeleza kama kiongozi wetu alivyoagiza, homngereni sana." Amesema Waziri Kikwete.

Aidha, amesema Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha uongozi, amejitahidi kuhakikisha vijana wanafunguliwa fursa na kuwezeshwa, ambapo amekitaka Kikundi hicho pamoja na Wanufaika wengine kutumia fedha hizo kwenye miradi yenye tija na kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine vinufaike na mikopo hiyo.

Mhe. Kikwete amempongeza Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Mhe. David Silinde kwa kuhakikisha maono ya Mhe. Rais Samia yanatafsiriwa kwa vitendo na kuwaletea maendeleo Wananchi.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika mkoa huu hali inayo chochea mapato ambayo husaidia Halmashauri kupata mapato na kuweza kutoa mikopo ya Asilimia 10 kutokana na mapato ya ndani.

Kikundi cha Vijana Chipaka kilichopo Mtaa wa Nyerere Kata ya Chipaka kimeanzishwa mwaka 2021 na kina Wanachama sita kwa mwaka 2024/2025 kimekopeshwa shilingi milioni 90 kwa ajili ya mradi wa kufuga na kuuza mayai.

Matukio katika Picha:

Picha zote juu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) alipotembelea na kukagua Kikundi cha Vijana cha Ufugaji Kuku na Uuzaji wa Mayai cha Chipaka wakati wa ziara yake ya siku moja Halmashauri ya Mji Tunduma wilayani Momba aliyoifanya tarehe 25 Februari 2025.

Picha zote juu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) akisalimiana na Viongozi na Watumishi mbalimbali mara baada ya kuwasili Halmashauri ya Mji Tunduma, kutembelea na kukagua Kikundi cha Vijana cha Ufugaji Kuku na Uuzaji wa Mayai cha Chipaka wakati wa ziara yake ya siku moja katika Halmashauri hiyo iliyopo wilayani Momba aliyoifanya tarehe 25 Februari 2025.

Matukio katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) alipotembelea na kukagua Kikundi cha Vijana cha Ufugaji Kuku na Uuzaji wa Mayai cha Chipaka wakati wa ziara yake ya siku moja Halmashauri ya Mji Tunduma wilayani Momba aliyoifanya tarehe 25 Februari 2025. (Picha zote na Benton Nollo).












Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa