• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

Imewekwa : March 15th, 2023

Halmashauri ya Mji Tunduma imegawa jumla ya lita 500 za maziwa sawa na pakiti 2000 zenye thamani ya shilingi 1,000,000/= kwa wanafunzi wa shule za Msingi.

Jumla ya wanafunzi 2000 wa Shule ya Msingi Mapande na Katengele wamepatiwa maziwa hayo Ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi kupitia unywaji wa maziwa.

Shirika la Afya Duaniani (WHO), linapendekeza kila mtu anywe angalau lita 200 za maziwa kwa mwaka ingawa wastani kwa dunia ni lita 108.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zinazokabiliwa na changamoto ya kuwa na watoto wenye udumavu, ugojwa ambao unachangiwa kwa kiwango kikubwa na lishe duni wanazozipata watoto walio chini ya miaka mitano. Sababu kubwa inayofanya watoto hao kudumaa ni ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Maziwa yana virutubisho vyote muhimu kwa ujenzi wa afya ya binadamu kwani yana protini ya daraja la kwanza, mafuta, madini, vitamin na sukari ya asili ya lactose na maji.

Jambo hilo linaifanya Halmashauri ya Mji Tunduma kuingia kwenye kampeni ya kuhamasisha unywaji wa maziwa kwa shule za msingi na Sekondari zote. Kampeni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndugu Lusajo Mwalukasa ambaye sasa anazunguka na walaamu wa Divisheni yake katika shule mbalimbali huku akitoa elimu juu ya unywaji wa maziwa huku wakigawa maziwa kwa wanafunzi hao

“Tunataka walau unywaji wa maziwa ufikie asilimia 60, watu waone umuhimu wa kunywa maziwa kwa sababu ni muhimu kwa afya zao, ndio maana tumeona tuanze na wanafunzi ili wawe mabalozi wazuri katika kuwaelimisha wazazi juu ya unywaji wa maziwa majumbani mwao” anasema Lusajo Mwalukasa

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mpande, Josephat Makange anasema uamuzi wa Halmashauri kufanya kampeni ya unywaji maziwa unapaswa kuungwa mkono na wadau wengine ikiwamo Mashirika, taasisi na wafanyabiashara, ili kuwakumbusha wazazi kujenga utamaduni wa kununua maziwa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto.

Baadhi ya wanafunzi wanakiri kuwa wengi wao hawajawahi kunywa maziwa wakiwa nyumbani.

“Nyumbani huwa sinywi maziwa kabisa kwa sababu wazazi hawaoni umuhimu huo ila wakielimishwa wanaweza kuanza kununua hata mara mbili kwa wiki,” anasema mwanafunzi Isaya Mwashiuya.

Mtaalamu wa Lishe wa Halmashauri ya Mji Tunduma Bwana Jonas Kamala anasema umuhimu wa maziwa mwilini ni mkubwa hasa kutokana na virutubisho vilivyopo. Anasema maziwa yanaweza kumfanya mtu kuwa na meno imara yanayong’aa, ngozi nyororo na ng’avu pia na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini pia maziwa yana madini ya Calcium yenye kazi kubwa ya kujenga mifupa na meno.

“Kwa hiyo uimara wa meno na mifupa hutegemea pia unywaji wa maziwa, ni vizuri familia kujiwekea mkakati wa kila mtu kupata maziwa,” anasema.

Anasema maziwa pia yana vitamini ‘D’ kwa wingi ambayo inaweza kupatikana kwa kuota jua hasa wakati wa asubuhi. Vitamin D inayopatikana kwenye maziwa husaidia utengenezwaji wa kichocheo cha Serotonin kinachohusisha masuala ya ‘mood’. Unaweza kupata hamu ya kula, kulala na wakati mwingine unywaji wa maziwa unaweza kupunguza uchovu na kumpa mtu raha.

Bwana Kamala anasema maziwa mazuri zaidi ni yale yatokanayo na wanyama kwani yana protini inayopatikana kwa kiwango cha hali ya juu.

Mtaalamu mwingine wa lishe Meckson Mandela anasema unywaji huo wa maziwa haupaswi kupita kiasi.

“Kunywa maziwa kiwango kile kinachotakiwa mwilini, usinywe maziwa mengi hasa krimu kwa sababu unywaji huo unaweza kukusababisha uzito kupita kiasi,” anasema Bwana Mandela

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa