• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Madiwani Ziarani Kahama na Mwanza

Imewekwa : December 5th, 2023

Na Benton Nollo, Tunduma TC

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Tunduma wamefanya ziara  katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa lengo la kubadilishana uzoefu ili kuboresha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi wa Tunduma na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ziara hiyo ya siku mbili ambayo imefanyika kwa nyakati tofauti tarehe 27 na 28 Novemba 2023 kwanza imelenga kujifunza masuala ya ukusanyaji wa mapato, pili udhibiti wa taka ngumu, tatu uhifadhi wa mazingira na nne ni usimamizi jadidi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Ayubu Mlimba amesema pamoja na kwamba Halmashauri hiyo ina mapato makubwa uongozi umeona ni vema kwenda kujifunza ili kuongeza ufanisi zaidi katika ukusanyaji wa mapato lakini pia kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi wa mji wa Tunduma.

“Viongozi wenzangu pamoja na kwamba Halmashauri yetu ina mapato makubwa, tumeona ipo haja ya kuja kwenu kujifunza mbinu na mikakati mnayoitumia katika ukusanyaji wa mapato ili na sisi tukaongeze juhudi na ili tufanye vizuri zaidi.” Amesema Mlimba.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa amesema amejifunza namna Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kahama wanavyoshirikiana na Wataalam na kuheshimu mipango inayotokana moja kwa moja na mawazo ya Wananchi.

“Nimejifunza wenzetu wanafanikiwa sana kwa sababu wanaheshimu mawazo yanayotokana na Wananchi…mipango yetu itokane na mawazo ya Wananchi…sis tupo hapa juu, Madiwani na Wataalam, sawa tunapanga lakini tunachokipanga lazima kitokane na Wananchi juu ya kile wanachokifikiria na kukihitaji ili kupata mpango wa maendeleo, tusitekeleze mipango ya maendeleo kutokana na jinsi tunavyoona kama Wataalam na Madiwanii bila kuwashirikisha Wananchi.” Amesema Magesa na kuomngeza:

“Wenzetu wana mradi ya Kimkakati wa bilioni 27 wa Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa kwa awamu awamu huku mapato yao ya ndani katika miradi ya maendeleo ni bilioni 3 tu, lakini sisi hatuna miradi kama hiyo na tuna bilioni 7 za mapato ya ndani katika miradi ya maendeleo, tumetawanya fedha kwenye miradi midogo midogo ambayo huwezi kuona ufanisi wake katika jamii…hii maana yake wenzetu wanakubaliana…hili ni fundisho kwetu.”

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba amesema siri kubwa ya mafanikio katika ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Waheshimiwa Madiwani na Wataalam.

“Sisi tulikaa tukakubaliana kuwa na miradi ya kimkakati licha ya kwamba mapato yetu ni kidogo…tuliwashirikisha Wananchi na tukaweka mazingira wezeshi kwao na tukafanikiwa…sasa hivi tunajenga Hospitali ya Manispaa kwa awamu ya bilioni 27 kwa mapato ya bilioni 3 kwa mwaka.” Amesema Msumba.

Aidha, katika siku ya pili ziara hiyo imefanyika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambapo Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalam wamejifunza namna Halmashauri hiyo inavyokusanya mapato, namna ya kubuni vyanzo vipya vya mapato, ukusanyaji wa mapato na jinsi mapato hayo yanavyotumika kutoa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya uwekezaji ambayo hugeuka kuwa vyanzo vya mapato.

Matukio katika Picha:



















Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa