• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

MAPENDEKEZO YA KUIPANDISHA HADHI HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA KUWA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TUNDUMA

Imewekwa : January 21st, 2023

Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kupitia Baraza la Madiwani sasa rasmi imeamua kuomba ridhaa ili iwe Manispaa ya Tunduma badala ya Halmashauri ya Mji Tunduma na hii ni kutokana na vigezo vingi vinavyoifanya Tunduma sasa kuwa na Hadhi hiyo. Baadhi ya Mambo yanayoifanya Tunduma kuomba kuwa Manispaa ni kama yafuatayo:-

1.1. Eneo na utawala

Halmashauri ya Mji wa Tunduma ipo katika mpaka wa Tanzania na Zambia, pia unapakana na wilaya ya Ileje upande wa Mashariki, Nchi ya Zambia na wilaya ya Momba kwa upande wa magharibi na wilaya ya Mbozi kwa upande wa Kaskazini ipo kusini magharibi mwa mkoa wa Songwe, kati ya latitudo 9003’ na 9023’ kusini mwa Ikweta na longitudo 32038’ na 320054’.

Halmashauri ya mji ipo umbali wa mita 1,400 hadi 1,650 kutoka usawa wa bahari, na inapata mvua ya wastani wa mm 1,350 -1.550 kwa mwaka.

Halmashauri ya Mji Tunduma ilianzishwa rasmi tarehe 1 Julai 2015 kufuatia tangazo la Serikali kwa GN namba 378.

Halmashauri ina kilometa za mraba 420, jimbo 1 la uchaguzi (Jimbo la Tunduma), Tarafa 1, Kata 15 na Mitaa 71.

1.2. Idadi ya watu

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Mji Tunduma ina jumla ya watu 122,622 kati ya hawa wanaume ni 58,860 na wanawake ni 63,762. Kwa Mwaka 2023, Halmashauri ya Mji wa Tunduma inakadiriwa kuwa na watu 170,026 kati ya hawa wanaume 78,309 na wanawake 91,717 na kiwango cha ukuaji (Growth rate) ni asilimia 6.7 zaidi ya kiwango cha ukuaji wa kitaifa wa 2.9%, wastani wa idadi ya watu katika kaya ni 4 na idadi ya kaya zilizopo ni 42,507.

2.0. HUDUMA ZA KIJAMII NA HALI YA KIUCHUMI

2.1. Huduma za Kijamii

Halmashauri ya Mji wa Tunduma ina jumla ya shule za Msingi 64 kati ya hizo Shule 49 ni za Serikali na Shule 15 zinamilikiwa na watu binafsi. Idadi ya Shule za Sekondari zilizopo ni 20 ambapo kati ya hizo Shule 14 zinamilikiwa na Serikali na shule 6 ni za binafsi.

Kwa upande wa Afya, Halmashauri ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 22 ambapo jumla ya vituo 13 vinamilikiwa na Serikali ikiwemo Hospitali 1, Vituo vya afya 5 na zahanti 7. Vituo vya kutolea huduma 9 vikiwemo vituo vya afya 2 na Zahanati 7 vinamilikiwa na Watu binafsi/Mashirika ya dini.

Halmashauri ya Mji Tunduma ina mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 220.18 kati ya hizo kilomita 183.18 zinahudumiwa na TARURA na kilomita 37 zinahudumiwa na wakala wa barabara Mkoa (TANROADS).

Vyanzo vya maji katika Mji wa Tunduma ni visima viefu. Hali ya upatikanaji wa maji kwa katika Halmashauri ya Mji Tunduma ni asilimia 89.45

2.2. Hali ya Uchumi

Tunduma ni Mji wa kibiashara hivyo idadi kubwa ya wananchi wanajishughurisha na biashara ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa (80%) katika kukuza uchumi wa Mji na kuleta maendeleo katika jamii. Kwa kiasi kidogo wananchi waliopo pembezoni mwa Mji ndio wanashughurika na kilimo cha mazao ya biashara, chakula na ufugaji. Mazao ya chakula yanayolimwa ni, mahindi, ulezi, maharagwe, mtama, mihogo na mbogamboga. Mazao ya biashara ni alizeti, karanga, maharagwe na mahindi. Pato la mtu linakadiriwa kuwa Tsh. 1,011,590.00 kwa mwaka.

3.0. VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA MANISPAA

3.1. Vigezo vya kuzingatia

Ili kuweza kuanzishwa/kupandishwa hadhi Halmashauri Mji kuwa Manispaa kuna vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya mwaka 2007, Kipengele cha Jedwali la Tano (The Urban Planning Act No 8 of 2007), (Item number 5 of the Fifth Schedule) kama ifuatavyo:-

i. Kuwe watu wasiopungua laki moja (100,000)

ii. Asilimia 30% ya wakazi wake wawe katika ajira isiyohusiana na kilimo(Nonagricultural Sector)

iii. Kuwe na walau kiwanda kikubwa kimoja (Manufacturing industry)

iv. Kuwe na viwanda kadhaa vya “Processing

v. Asilimia Sabini (70%) ya matumizi ya Manispaa yatokane na vyanzo vyamapato ya Halmashauri (Own Sources).

vi. Kuwepo na huduma za jamii zifuatazo:-

  • Kituo cha Elimu ya Watu Wazima;
  • Hospitali ya Rufaa;
  • Chuo Kikuu;
  • Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa;.na kiwe ni Kituo cha Taasisi za Kimataifa (Mult National organization.

Kutokana na kasi ya ukuaji wa halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe hususani katika shughuli za kimaendeleo yanayochochea ongezeko la uchumi kwenye Mji huo ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri hiyo inapendekeza kuipandisha hadhi ya Mji huo kuwa Manispaa.

Pendekezo hilo limetokewa mara baada ya kujadili mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2023/2024 yenye thamani ya shilingi billion 33.4 kwenye baraza la madiwani lililoketi January 21, 2023 ambapo wametumia baraza hilo kwa kuainisha vigezo na hali halisi ya Mji wa Tunduma jinsi ilivyo kwa Sasa.

Akisoma mapendekezo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Philemon Magesa, Afisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri Ndugu Belton Galigo amesema Mji wa Tunduma kwa sasa una zaidi ya wakazi laki 1.7 ambapo hiyo ni Moja ya kigezo wanachokizingatiwa lakini pia kuna uwepo wa huduma za kijamii kama vile vituo vya elimu ya watu wazima sanjari na hayo pia Mji huu una kumbi kubwa 4 zenye uwezo wa kuchukua watu 500 kila Mmoja.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Momba Fack Lulandala amesema wao kama Wilaya kwenye ngazi ya DCC wameridhia na wanaendelea kutoa ushauri ambao wanaimani utaenda kutekelezwa kwani Halmashauri hii inafanya vizuri sana hasa katika makusanyo yake ya ndani kupitia kazi zinazofanywa na madiwani na watendaji ambapo kwa mwaka 2023/2024 wamepangiwa kukusanya Billion 33,422,058,078.00

Wakichangia hoja za pendekezo hilo baadhi ya madiwani akiwemo Mhe. Frank Mponzi Diwani kata ya Majengo pamoja na Mhe. Qwintin  Kayombo Diwani wa kata ya Uwanjani wamesema wanabariki Mji wa Tunduma kupandishwa hadhi na kuwa Manispaa kwani itakuwa ni fahari kubwa ambapo watakuwa wameongeza huduma nyingi za kijamii lakini pia itasaidia kupanda kwa gawio toka Taifa.

Matangazo

  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili January 24, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • DC Mwandobo Akutana, Wamiliki wa Maegesho

    April 16, 2025
  • Vyombo vya Ulinzi, Usalama Vyaimarisha Ushirikiano

    April 16, 2025
  • TAMISEMI Yaomba Trilioni 11.8 Bajeti ya 2025/2026

    April 16, 2025
  • Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Serikali Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi

    April 11, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa