• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Mei Mosi Songwe Yafana

Imewekwa : May 1st, 2025

Na Benton Nollo, TTC

Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Meimosi) kwa mwaka 2025 mkoani Songwe yamefanyika katika Mji wa Vwawa, Wilaya ya Mbozi tarehe 01 Mei 2025 ambapo zimehudhuriwa na Wafanyakazi kutoka sekta na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo husherehekewa kila mwaka alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Farida Mgomi, aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo.

Akihutubia katika viwanja vya maadhimisho, Mhe. Mgomi amewataka Wafanyakazi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, kwa lengo la kuchagua viongozi bora watakaosimamia masilahi ya Wafanyakazi na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Aidha, alieleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuboresha na kusimamia vyema ustawi wa wafanyakazi kupitia hatua mbalimbali ikiwemo utoaji wa ajira mpya, uboreshaji wa mazingira ya kazi, pamoja na kulipa madeni na malimbikizo ya watumishi wa umma.

Katika hotuba yake, Mhe. Mgomi amesisitiza umuhimu wa nidhamu ya matumizi ya rasilimali kwa kuwaagiza waajiri wote kuepuka kuzalisha madeni mapya yasiyo na msingi, ambayo yamekuwa mzigo kwa Serikali.

Ameeleza kuwa ni muhimu kuhakikisha haki za Wafanyakazi zinalindwa kwa mujibu wa Sheria ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Vilevile, amezitaka Halmashauri zote ndani ya Mkoa wa Songwe kuhakikisha marekebisho ya mishahara yanatekelezwa kwa haraka pindi mtumishi anapopanda daraja, akisisitiza kuwa ucheleweshaji wa mchakato huo huchangia kuibua madeni yasiyo ya lazima.

Akihitimisha hotuba hiyo, Mhe. Mgomi amewakumbusha waajiri wote kuzingatia misingi ya haki, sheria na kanuni katika kushughulikia masuala ya masilahi ya watumishi.

Maadhimisho hayo yalipambwa na maandamano ya amani, burudani kutoka kwa vikundi vya sanaa, pamoja na maonyesho ya shughuli mbalimbali za wafanyakazi kutoka sekta tofauti, na kuhudhuriwa na viongozi wa kisiasa na wa vyama vya wafanyakazi.

Matukio katika Picha:

(Picha Benton Nollo na Julius Evandino, TTC).

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa