• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Mhe. Mlimba: Tukishirikiana Tutaokoa Maisha ya Watanzania

Imewekwa : November 10th, 2023

Na Benton Nollo, Tunduma TC

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayubu Mlimba amelishukuru Shirika la Amref kupitia Mradi wa USAID Afya Shirikishi kuhusu kuimarisha ushiriki wao katika kuboresha uelewa na huduma za Kifua Kikuu katika Halmashauri hiyo ambapo amebainisha kuwa kwa ushirikiano huo, afya na maisha ya Wananchi wa Tunduma yataokolewa dhidi ya maradhi hayo.  

Mhe. Mlimba ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Waheshimiwa Madiwani kuhusu ushiriki wao katika kuboresha uelewa na huduma za Kifua Kikuu katika Halmashauri hiyo, mkutano ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 10 Novemba 2023.

“Waheshimiwa Madiwani mnakumbuka mwaka jana wenzetu hawa walikuja, tulijifunza na lengo la mafunzo yoyote yale ni lazima yawe na mrejesho, ili kujitathmini kuona kama leo tunapokutana tena je, kuna mafanikio katika mapambano ya kuzuia ugonjwa huu tangu mwaka jana tulipopata uelewa…hili ni jambo la msingi sana kwetu sisi kama viongozi wa kijamii.” Amesema Mhe. Mlimba na kuongeza;

“Viongozi wenzangu pamoja na ninyi wawezeshaji, lengo la Mheshimiwa Rais Samia ni kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na afya njema wakati wote, kwa kuwa ukiwa na wananchi ambao afya zao siyo njema kwa hiyo hata uchumi hauwezi kusonga mbele, kwa hiyo kama lengo ndo hilo kuna haja basi tunapopeana mafunzo kama hayo, ni vema tukapeana mrejesho wa kile tulichojifunza na tumekwenda kufanya kazi ya kuwahamasisha Wananchi njia sahihi za kuepukana na maradhi haya.”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Selemani Kateti amelishukuru Shirika la Amref kwa kushirikiana na Kituo cha Maendeleo ya Mawasiliano Tanzania - TCDC kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kupata mrejesho wa mafunzo ya awali yaliyofanyika mwaka jana (2022).

“Kikao chetu cha leo kitatusaidia sana kupata mrejesho, kwanza wa maazimio yale ambayo tulikubaliana katika kikao kilichopita, lakini kuangalia mikakati ile tuliyotumia kuhakikisha tunapata mrejesho tegemewa na hasa ukizingatia Waheshimiwa Madiwani hawa ndiyo wanatoka kwenye jamii na ndiyo wanashiriki shughuli mbalimbali kama wawakirishi wa Wananchi kwenye jamii zetu.” Amesema Kateti na kuongeza;

“Pia, kikao hiki kitatusaidia kutengeneza maazimio mapya na mikakati mipya kwa namna ambayo Serikali na Wafadhili wamedhamiria katika kukabiliana na Ugonjwa wa Kifua Kikuu.”

Kateti amesema kuwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu ni hatari lakini una nafuu kwa kuwa unatibika hasa Wagonjwa wakizingatia maelekezo ya Madaktari na Wataalam wengine wa afya fotauti na magonjwa mengine.

Hivyo, Kateti ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani kama Wawakirishi wa Wananchi kutumia fursa hiyo kujielimisha vizuri ili kwenda kuhamasisha wananchi kujitokeza katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya kupima afya zao ili wale wanaobainika kuwa na bakteria wa ugonjwa huo waanze tiba mapema.

Naye, Mratibu wa Mradi wa USAID Afya Shirikishi wa Amref Mkoa wa Songwe, Dkt. Malneste James amesema amesema mradi huo umejikita zaidi kwenye jamii kwa kuwa kuna wananchi wanaumwa lakini hawawezi kufika katika vituo vya kutoa huduma za afya kwa sababu mbalimbali ikiwemo umbali.

“Sisi kama Wadau tulikaa na kubaini kuwa pamoja na kuboreshwa kwa huduma za afya zinazotolewa sasa hivi na Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika huduma za afya nchini lakini bado kuna changamoto katika baadhi ya maeneo ikiwemo upungufu wa rasilimali watu na rasilimali fedha.” Amesema Dkt. James.    

Dkt. James ameishukuru Serikali kwani moja ya maazimio ya kikao kilichopita ni kwamba Waheshimiwa Madiwani waliazimia huduma za Mionzi kwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu ziwe bure na hilo limetekelezwa.

Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Mji Tunduma, Dkt. Enock Mwambalasa amesema kutokana na mchango wa Wahudumu Ngazi ya Jamii hali ya maambukizi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu umepungua hadi kufikia wagonjwa 138 mwaka huu 2023 ukilinganisha na wagonjwa 252 mwaka 2022.


Matukio Katika Picha:

Matangazo

  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili January 24, 2025
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 January 23, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Waziri Aweso Aagiza Mradi wa Maji Tunduma, Vwawa Kukamilika kwa Wakati

    March 20, 2025
  • 'Ahadi Imetimia, Bilioni 119.9 Kutumika Mradi wa Maji Tunduma, Vwawa'

    May 20, 2025
  • Wananchi Wanatarajia Uongozi Bora Kutoka Kwenu: DC Mwandobo

    March 05, 2025
  • Tusisahau Tulikotoka: TD Chaurembo

    March 05, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa