• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Mikopo ya Asilimia 10 Kutolewa kwa Mtu Mmoja Mmoja

Imewekwa : March 8th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Marry Chatanda amesema mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri sasa itaanza kutolewa kwa mtu mmoja mmoja tofauti na awali ambapo ilikuwa ikitolewa kwa vikundi vya kuanzia watu watano kwa makundi maalum ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.

Chatanda ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia Wanawake na Wananchi wa Mkoa wa Songwe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yalifanyika katika Halmashauri ya Mji Tunduma kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma tarehe 08 Machi 2024.

Kiongozi huyo wa UWT Taifa amefafanua kuwa mikopo hiyo itarejea tena hivi karibuni baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na wanufaika kutofanya marejesho kwa wakati na kuilazimu Serikali kusitisha kwa muda mwezi Aprili 2023 ambapo sasa itaruhusu mtu mmoja mmoja kupata mikopo hiyo.

“Kina mama wenzangu ili tuweze kuepukana na mikopo zembe inayoitwa kausha damu, Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuwa mikopo ya asilimia 10 za mapato ya ndani ya Halmashauri irejee tena na sasa itolewe hata kwa mtu mmoja mmoja.” Alisema Chatanda ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo.

“Aidha, nitoe wito kwa wanawake kutumia fursa nyingine mfano Baraza la Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi kama Benki ya Kilimo na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ili kuepuka kudhalilika na mikopo yenye masharti magumu inayotolewa kiholela”. Aliongoza Chatanda.

Aidha, Chatanda alizungumzia suala la malezi kwa watoto kwa kuwataka wazazi kuzingatia lishe ambapo ameupongeza Mkoa wa Songwe kwa kufanya vizuri katika kuhakikisha watoto wanapata lishe bora.

Vile vile,  Chatanda amewaasa wazazi kuimarisha maadili ya watoto wao kutokana na utandawazi ambao unasababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa kuwa wazazi wengi wamesongwa na kutingwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kazi za maofisini, uzalishaji mali na biashara huku wakiwaacha watoto bila uangalizi hali ambayo ni hatari kwa usalama wa watoto katika makuzi yao.

“Akina mama tumewaacha watoto wanajilea wenyewe kupitia utandawazi, tunaacha watoto wanachezea simu mpaka wanaona mambo ya kidunia ambayo hayawahusu kutokana na umri wao, mambo ambayo yanasababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu.” Alisema Chatanda na kuongeza;

 “Wazazi turejee kwenye utamadumi wetu za kitanzania tukae na watoto wetu tuwaeleze masuala ya maendeleo ya kijamii, mila na desturi zetu ili tuokoe kizazi chetu kinachoangamia kwa kukosa malezi bora.”

Chatanda ameeleza jitahada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwainua wanawake ikiwemo kuimarisha sekta ambazo zinawagusa wanawake moja kwa moja mfano sekta ya maji, afya, kilimo, elimu na miradi ya kimkakati pamoja na kuhuisha majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ambayo aliyaasisi mwaka 2016 akiwa makamo wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Chatanda amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni ”Waekeza kwa Wanawake, Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii”, inachagiza kutoa msukumo kwa wadau wote wa masuala ya wanawake, kuwekeza kwa wanawake ili kuhamasisha na kuharakisha maendeelo ya Taifa na kwamba kauli mbiu hiyo inashabihiana na kilichofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu kuingia madarakani mwaka 2021.

Taasisi za umma, vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo TANESCO, NMB, STAMICO, IRDO, Solidalidad, TRA, UWT, TAKUKURU, Mahakama ya Tanzania Mkoa wa Songwe, Wakala wa kilimo, Tanroads Songwe, Shalom, Wakala wa maji na usafi wa Mazingira, Tanzania Women Chamber of Commerce, Mtandao wa Askari Wanawake, Majeshi ya Ulinzi na Usalama na vikundi vya wanawake wajasiliamali wameshiriki maadhimisho hayo.

 Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 1975 huko Marekani na kisha mwaka 1977 Umoja wa Mataifa ulialika mataifa wanachama ikiweno Tanzania kuitambua tarehe 8 Machi kuwa ni siku ya haki za wanawake na amani.

Matukio katika Picha:





Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa