• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

MKUU WA WILAYA YA MOMBA AZINDUA MWONGOZO WA UTEUZI WA VIONGOZI WA ELIMU PAMOJA NA VITABU VYA MIKAKATI YA KUBORESHA UENDESHAJI WA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI

Imewekwa : September 30th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Lulandala alisema Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeandaa Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Vitabu vya Mikakati ya kuboresha uendeshaji wa Elimu Msingi na Sekondari Nchini, vyote vikiwa na Lengo la kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu msingi na Sekondari katika ngazi za Shule, Kata, Halmashauri na Mikoa.

Tutakumbuka tarehe 04/08/2022 Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (M), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Mkoani Tabora alizindua Mwongozo wa uteuzi wa Viongozi wa Elimu pamoja na vitabu vya mikakati ya uendeshaji wa elimu Msingi na Sekondari huku kukuwa na maelezo mahususi kwetu kama watendaji wa Serikali kwa ngazi tofauti kufuatia changamoto zilizobainishwa katika Uboreshaji Elimu msingi na Sekondari na kuzipatia ufumbuzi kwenye maeneo yetu.

Katika maelekezo yake Mkuu wa Wilaya alisema kuwa:-

Kwa kuanza na mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu, huu umeweka bayana taratibu za uteuzi wa viongozi wa Elimu katika ngazi za Shule, Kata, Halmashauri na Mikoa. Hivyo, malengo mahususi ya mwongozo huu ni pamoja na kubainisha sifa za uteuzi wa viongozi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa. Mwongozo umeeleza taratibu za uteuzi wa viongozi hao na kubainisha hatua za kuchukuliwa na Mamlaka za Uteuzi wakati wa kutengua viongozi pale inapolazimu kufanya.

Pili, Mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimu Msingi, umeainisha jukumu la Ofisi ya Rais TAMISEMI la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Sera, Sheria na Miongozo ya Elimu ya Msingi na Sekondari inayotolewa na Serikali katika kuimarisha utoaji wa Elimu nchini. Sekta ya Elimu na Mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo ya Taifa 2011/2012 hadi 2024/2025, inatarajia kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati.

Aidha, Uchambuzi wa maendeleo ya usimamizi wa elimu nchini umebaini uwepo wa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na:-

  1. Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaofaulu kuingia Kidato cha Kwanza kutoka asilimia 30 mwaka 2012 hadi asilimia 81 mwaka 2021.
  2. Ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano kutoka Kidato cha nne kutoka asilimia 9 mwaka 2012 hadi asilimia 35 mwaka 2021.
  3. Ongezeko la Idadi ya wanafunzi wa shule za Msingi kutoka 8,639,202 mwaka 2016 hadi 11,196,788 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 22.84.


Pamoja na mafanikio yaliyobainika kwenye Sekta ndogo ya Elimu msingi, changamoto kadhaa zimebainika ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa uchache ikiwa ni pamoja na:-

  1. Mdondoko wa wanafunzi wa darasa la III hadi VI
  2. Ukosefu wa chakula shuleni
  3. Baadhi ya wanafunzi kuhitimu Darasa la saba bila kumudu stadi za Hisabati na English Language.
  4. Msongamano wa Wanafunzi madarasani.
  5. Upungufu wa Walimu.
  6. Ufuatiliaji dhaifu wa ufundishaji katika Madarasa ya awali, la I na II
  7. Baadhi ya wanafunzi kujiunga darasa la I bila kupitia Elimu ya awali,
  8. Umbali mrefu wa kwenda shule na kurudi nyumbani,
  9. Upungufu wa Miundombinu ya Elimu ya awali na Msingi
  10. Baadhi ya wanafunzi kujihusisha na biashara ndogondogo.


Niwatake mpitie mkakati huu ili mzifahamu vyema changamoto hizo ambazo zimeanishwa kuanzia ukurasa wa 13 hadi ukurasa wa 52 ambapo mtazifahamu, mtajua athari zake, mtatambua fursa, mtapanga mikakati ya utatuzi na mtafahamu viashiria vya mafanikio sambamba na kujiwekea mpango wa kutathimini utekelezaji wa mikakati ya kumaliza changamoto hizo.

Mbali na chamgamoto zilizoanishwa, mkakati umeainisha jumla ya malengo matano yenye lengo la kuhakikisha utekelezaji wa Elimu Msingi unatoa matokeo yaliyokusudiwa. Ni matumaini yetu kama Halmashauri kuona kwenye kila lengo kunafanyika maboresho kwa kadri ya changamoto zinavyojitokeza. Malengo hayo ni

  1. Kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa na kukamilisha mzunguko wa elimu msingi;
  2. Wanafunzi wote wanaomaliza Darasa la Pili wamudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu;
  3. Wanafunzi wote wa rika lengwa wanaojiunga Darasa la Kwanza wawe wamepitiaElimu ya Awali;
  4. Kuongeza idadi ya wanafunzi wa sekondari wanaochagua Kusoma Masomo ya Sayansi na ya Michepuo; na
  5. Kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya elimu msingi. Changamoto zinazokabili kila eneo lakipaumbele zimeainishwa.


Aidha katika kufikia malengo hayo kama yalivyoainishwa kwenye Mkakati wa Kuimarisha ujifunzaji, inahitajiaka nguvu ya pamoja inayojumuisha Wadau mbalimbali kwa kuanzia na Wizara ya Elimu Sayasi na Teknolojia, Wanasiasa, OR-TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati na Bodi za Shule, Wazazi/Jamii, Walimu, Wanafunzi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Wafadhili.

“Nitoe rai kwetu sote kuhakikisha tunashirikiana ili kutekeleza kwa vitendo Azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kuimarisha Ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuwa na Wahitimu wenye umahiri uliokusudiwa” alisema Mhe. Fakii

Eneo la tatu la muhimu katika Uboreshaji Elimu Msingi na Sekondari ni hatua mbalimbali zinazochukuliwa na zinazopaswa kuchukuliwa na Serikali katika ngazi zote kuboresha elimu nchini, ili kuondoa changamoto zinazokwamisha ufundishaji na ujifunzaji shuleni

Katika kuzindua rasmi Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu pamoja na Vitabu vya Mikakati ya kuboresha uendeshaji wa elimu msingi na sekondari katika Halmashauri yetu ya mji Tunduma, mambo yafuatayo tunapaswa kuyazingatia:-

  1. Kila Kiongozi wa Elimu katika ngazi ya shule, Kata na Halmashauri afuatilie ufundishaji na ujifunzaji shuleni na kushauriana na walimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata umahiri uliokusudiwa kwa masomo yote, badala ya kukaa Ofisini:
  2. Kila mwalimu aweke malengo yake binafsi katika masomo anayofundisha na kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayeshindwa kupata umahiri uliokusudiwa katika somo lake ifikapo mwishoni mwa kila mwaka.

 

Mkurugenzi na viongozi wa elimu katika ngazi za Kata hakikisheni kuwa: -

  1. Walimu wanatambuliwa hadhi yao, wanatiwa moyo kulitumikia Taifa lao na hawadhalilishwi na mtu yeyote,
  2. Wazazi wahamasishwe kuthamini kazi ya walimu kwa vitendo pamoja na kushirikiana vizuri na walimu katika suala la malezi ya Watoto wawapo shuleni na nyumbani,
  3. Viongozi wa elimu wajielekeze zaidi kufuatilia ufundishaji wa walimu darasani na kutatua kero za walimu kwenye maeneo yao ya kazi (yaani shuleni),
  4. Uteuzi wa viongozi wanaopewa dhamana ya kusimamia elimu msingi na sekondari katika ngazi za shule, Kata na Halmashauri uzingatie umahiri, weledi, ubunifu na uzoefu kama ilivyobainishwa kwenye Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi ulioandaliwa na
  5. Viongozi wa Elimu katika ngazi zote mkatekeleze mikakati hii ya uboreshaji elimu iliyoandaliwa ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika Elimu Msingi na Sekondari.


Aidha,Watendaji wa kata mkishirikiana na Maafisaelimu kata mnapaswa kwenda kusimamia na kuhakikisha miongozo na vitabu vya maboresho ya elimu inazinduliwa na kufikishwa kwa mamlaka zilizoko chini yenu ( Kata, Mitaa na Shule) mapema kabla ya mwezi Novemba 2022 kuisha. Aidha tukawe wabunifu wa kutumia fursa ya rasilimali zinazopatikana kwenye maeneo yenu ili kufikia malengo, sambamba na watendaji wa kata/maafisaelimu kata kuwasilisha mpango wa utekelezaji wa mikakati hii na taarifa ya utekelezaji wa kila robo mwaka.

Kwa kuhititimisha hotuba yangu, mikakati hii imebainisha changamoto sambamba na njia za utatuzi kwa kila changamoto ili kurahisisha utekelezaji wake, niwaombe tukaipitie kwa makini na tuone tija yake. Pia tukazingatie mwongozo wa uteuzi wa viongozi wa Elimu ili kuwezesha kupata Viongozi bora katika ngazi za Shule, Kata na Halmashauri kwa kuzingatia Weledi, Ujuzi, Uzoefu na Ubunifu na bila upendeleo, huba na kwa kujuana.

Suala la kuboresha Elimu ya Tanzania ni jukumu letu sote, Kila mmoja wetu kwa nafasi yake ana mchango wa kuboresha Elimu kwa ajili ya kupata rasilimali watu mahiri watakaotumika kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu. Rai kwa kila mmoja wetu kuonesha uzalendo, uchapakazi ushirikiano wa hali ya juu katika suala hili la kuboresha elimu shuleni.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa