• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Mnao Wajibu Kuwasimamia CHWs: DC Mwandobo

Imewekwa : May 20th, 2025

Na Benton Nollo, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Elias Mwandobo amewaagiza Watendaji wa Kata wote Halmashauri ya Mji Tunduma kuwasimamia ipasavyo Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii - CHWs, kuwatembelea na kutoa elimu ya masuala ya lishe kaya zenye Wajawazito na Watoto wadogo chini ya miaka mitano ili kuifanya jamii kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu lishe ambapo kwa kufanya hivyo afya zao zitakuwa bora.

Mhe. Mwandobo ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Kamati ya Tathmini ya Lishe Ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 20 Mei 2025.

" Watendaji wa Kata nyie ndiyo mnao wajibu wa kuwasimamia CHWs katika maeneo yenu ili watembelee kaya zenye Wajawazito na Watoto Chinese ya miaka mitano kwa lengo la kutoa elimu ya masuala ya lishe maana hapo ndipo kwenye msingi wa kujenga jamii yenye afya bora ya baadaye." Amesema Mhe. Mwandobo.

Aidha, Mhe. Mwandobo amesisitiza suala la uchangiaji chakula shuleni, kwamba kwa kuwa msimu huu ni wamavuno Watendaji  wa Kata wahamasishe ukusanyaji wa chakula kutoka kwa Wazazi lakini pia waimarishe usimamizi wa matumizi ya chakula kinachopatikana, ili kuleta hamasa kwa Wazazi kuendelea kuchangia wakiwa na uhakika chakula kinachopatikana kinatumika ipasavyo.

Kwa upande wake Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Tunduma, Frida Muhindi akizungumza alipokuwa akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Afua za Lishe, kwa kipindi hicho katika kiashiria cha CHWs kutembelea kaya zenye Wajawazito na Watoto wadogo chini ya miaka mitano, kaya 13,227 zilitembelewa ambapo Kaya 8,964 zilikuwa na Wajawazito na Watoto wadogo huku Wazazi na Walezi wenye Watoto wa miezi 0 - 23 wapatao 4,307 walipatiwa unasihi wa ulishaji wa Watoto wadogo.

Kwa kiashiria cha idadi ya watoto wanaokula chakula shuleni imeongezeka hadikufikia asilimia 82.97 ukilinganisha na asilimia 79.73 robo ya pili huku kiashiria cha maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe kwenye Mitaa kimefanyika vizuri na kwa wakati.

 Pia, kiashiria cha utoaji wa fedha kwa Halmashauri zimetolewa shilingi milioni 110 kati ya shilingi milioni 142.7 sawa na asilimia 77.07.

Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa