• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Msenjelwa Awaapisha Wajumbe Kamati ya Huduma ya Mikopo Ngazi ya Kata, Kupatiwa Mafunzo

Imewekwa : October 7th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Hakimu Mkazi Mwandamizi Wilaya ya Momba, Claudi Msenjelwa (pichani) amewaapisha Wajumbe wa Kamati ya Huduma ya Mikopo ya Asilimia Kumi (10%) Ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Mji Tunduma, kwa ajili ya kujengewa uwezo kuhusu Kanuni na Mwongozo wa Usimamizi wa Utoaji wa Mikopo hiyo tukio ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 07 Oktoba 2024.

Msenjelwa amewaasa Wajumbe hao kuzingatia kiapo chao kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao wakati wa mchakato wa utoaji wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%) kwa Makundi yanayonufaika na mikopo hiyo ambayo ni Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.

"Ndugu Washiriki niwaombe mtambue kuwa mnapaswa kuishi kiapo chenu kwa sababu yeyote atakayekwenda kinyume na kiapo hiki Sheria itachukua mkondo wake hivyo mnapaswa kufuata taratibu zote za utoaji wa mikopo hii kwa uadilifu mkubwa.” Amesema Msenjelwa na kuongeza;

“Ni lazima tuhakikishe kwamba mwongozo wa Usimamizi na Utoaji wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu unafuatwa ili walengwa waweze kunufaika kwa haki na si vinginevyo."

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma, Mwanaishamu Nassor alisema mafunzo kwa Wajumbe hao ni ya siku moja na yanahusu kujua malengo na umuhimu wa mwongozo wa Usimamizi na Utoaji wa Mikopo ya Asilimia Kumi (10%) kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Nassor alisema Wajumbe watajifunza kuhusu Kanuni na Taratibu za Utoaji wa Mikopo ya Vikundi ambapo ndani yake watajifunza kuhusu Kanuni za usimamizi na utoaji wa mikopo, viwango vya ukomo wa utoaji wa mikopo, kikundi kuhitimu kunufaika na mikopo pamoja na orodha ya vitu vya kuzingatiwa wakati wa kufanya tathmini ya kikundi kuhitimu kunufaika na mikopo.

Pia, Nassor alisema hatua za uundaji wa vikundi ni moja ya mambo ambayo Wajumbe hao watajifunza ambapo wataelekezwa kuhusu utambuzi wa vikundi na wajibu wa vikundi.

Kadhalika, Nassor aliainisha kuwa Wajumbe watafundishwa kuhusu muda wa kushughulikia maombi ya mikopo, mikopo ya vifaa, urejeshwaji wa mikopo, utaratibu wa ufuatiliaji na ukusanyaji wa marejesho kwa Mfumo wa Serikali Ulioboreshwa, utaratibu wa marejesho kwa Mfumo wa Serikali Ulioboreshwa, kuchelewesha na kushindwa kurejesha mkopo pamoja na matumizi ya fedha za mikopo kwa wanakikundi.

Pamoja na mambo mengine, Wajumbe walielekezwa kuhusu muundo na majukumu ya Wasimamizi wa Mikopo Ngazi ya Kata, ufuatiliaji na tathmini ya hali halisi ya kikundi kinachoanza kupata mikopo.

Aidha, Wajumbe walielezwa kuwahamasisha Wananchi hasa makundi hayo kujitokeza kupata mafunzo muda utakapowadia kwani Halmashauri ya mji Tunduma mpaka kufikia mwezi Septemba 2024 inazo shilingi bilioni 4.1 ambazo zinatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo kwa ajili ya mikopo hiyo ya Asilimia Kumi.

Ambazo amesema mpaka kufikia tarehe 30 Oktoba 2024 zinatakiwa kuwa zimeshakopeshwa kwa makundi hayo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Nassor ameeleza kuwa sababu iliyosababisha mikopo ya Asilimia Kumi (10%) kusimama kwa muda ilikuwa ni kufanya maboresho ya kanuni za utoaji mikopo ili mikopo inayotolewa iwe na tija kwa jamii.

"Maboresho yamefanyika katika suala la umri kwa upande wa vijana ambapo kwa sasa umri wa kijana umeongezeka kuanzia miaka 18 hadi miaka 45 wakati awali kigezo kilikuwa ni kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 35 hivyo, marekebisho hayo yameongeza wigo kwa vijana wengi kupata mikopo hii.” Amesema Nassor.

Nassor amefafanua kuwa kigezo kingine kwa wanakikundi kupata mkopo huo ni kuwa na namba ya NIDA kwani uwepo wa namba hiyo utarahisha upatikanaji wa taarifa muhimu za mkopaji katika mfumo.

Ameongeza kuwa ili kuongeza ufanisi zaidi wa utoaji wa mikopo, Divisheni ya Maendeleo ya Jamii itafanya ukaguzi wa andiko la biashara husika, soko pamoja na kuangalia uhalisia wa biashara kabla ya kutoa mikopo kwa wakopaji kwani hii itasaidia kupunguza hasara kwa wanufaika wa mikopo hiyo.

Nassor amesisitiza wakopaji wote wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%) watatakiwa kuhakikisha kuwa wanarejesha kwa wakati marejesho yao ili kutoa nafasi ya watu wengine kukopa.

Mikopo ya Asilimia Kumi (10%) hutolewa kila robo mwaka kwa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu, ili kuwasaidia kujiinua kiuchumi.

Matukio katika Picha:

(Picha Zote na Julius Evandino, TTC).


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mei Mosi Songwe Yafana

    May 01, 2025
  • Chaurembo Awapongeza Walimu

    April 30, 2025
  • Tunduma kwa Taaluma Sina Mashaka Nanyi: RAS Seneda

    April 30, 2025
  • Chaurembo Afungua Mafunzo Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili

    April 29, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa