• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

NMB TUNDUMA YAFUNGA MWAKA KIVINGINE

Imewekwa : June 20th, 2022

Benki ya NMB Tawi la Tunduma imefanya kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya maboresho ya huduma za kibenki zinazoendelea hususani katika mapinduzi ya kidigitali

Akieleza mapinduzi hayo meneja wa Benki ya NMB tawi la Tunduma Bwana Michael Mzinga alisema kuwa kwa sasa Banki ya NMB imebadilika na kuwa ya kidigitali na mteja haitaji kufika banki ili kupata huduma.

“Kwasasa unaweza kupakua huduma ya NMB MKONONI ambayo unaweza kufanya huduma zote ambazo ulitakiwa kuja ndani ya benki"

Bwana Mazinga aliendelea kueleza kuwa kwa sasa unaweza kuwa na KADI ambayo inakuwa na mkopo ndani yake. Kadi hiyo inaweza kutumika kwa kutoa pesa na kupokea huku ikiwa ni mkopo ambao mtumijia anaweza kuendelea kulipa kwa awamu hadi mkopo utakapo isha

Kwa upande wake Bwana Steven Mwasomola amabaye ni Afisa Mahusiano aliwaeleza watumishi kuwa kwa sasa Benki imeanzisha mikopo ya kilimo kwa ajili wa watu wote wanaojishughulisha na kilimo hivyo ni fursa mpya kwa wateja wa NMB kama kuna wakulima wanakaribishwa kuomba mikopo hiyo.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Bwana Philemon Magesa aliwashukuru sana NMB tawi la Tunduma kwa kuandaa kikao kazi hicho kilichoendana na chai kwani hakijawahi fanyika hivyo kuwa cha kwanza kwani Watumishi wa NMB wameacha Ofisi zao na kuwafuata wateja wao.

Katika maombi yake kwa Benki ya NMB tawi la Tunduma Bwana Magesa aliiomba Benki hiyo kusaidia katika Nyanja za Elimu kwani Tunduma ni Mji unakua sana hususani katika kipengele cha kuzaliana

“kwa mwaka watoto wanaozaliwa katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma ni Zaidi ya 500 ambao ni sawa na shule moja, hivyo japo kuwa tunajitahidi kujenga shule nyingi lakini bado tunazidiwa kwa idadi hii ya watoto wanao zaliwa kila mwaka”

Pia Mkurugenzi Magesa aliiomba banki hiyo kuweka TAWI katika jengo la utawala linalojengwa na linatarajiwa kuanza katumika Julai 1 mwaka huu.

“Tunakuomba ulete tawi katika jengo letu la Utawala, chumba kipo tunakupatia wewe uje kwa ajili ya kukiangalia na ilikifanyiwe marekebisho kwa ajili ya huduma za kibenki”

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya momba Bi. Marry Marco aliwashukuru sana NMB na kuwaomba waendelee kujitolea na kuunga mkono miradi ya maendeleo kwani licha tu ya watumishi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kupokelea mishahara yao katika Bank ya NMB bado pia mapato ya Halmashauri ya Mji yote yanapokelewa kupitia Benki yao, mfano kwa mwaka wa fedha huu hadi kufikia tarehe 16.06.2021 Halmashauri imekusanya mapato yake Tsh. 8,106,420,362.77/= ambazo zote zimepitia Benki ya NMB tawi la Tunduma

Bi. Marry aliendelea kusema kwamba Benki ya NMB tawi la Tunduma wamefanya jambo la mfano wa kuigwa kwa kuwatambua wateja wao na kuwapatia nafasi ya kuzijua fursa zinazotolewa nahivyo kuwaomba wasiishie hapo waendelee kwa makundi mengine ili wazidi kupata uelewa wa fursa zinazopatikana Benki ya NMB tawi la Tunduma

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa