• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

RC Chongolo Aridhishwa, Ujenzi wa Bwalo Dkt. Samia SH

Imewekwa : April 10th, 2025

Benton Nollo na Atwiya Mohamed, TTC.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe.Daniel Chongolo, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Bwalo la Chakula linalojengwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia SH iliyopo Kata ya Namole, Halmashauri ya Mji Tunduma, wilayani Momba.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya katika Halmashauri hiyo tarehe 10 Aprili 2025, mara baada ya kukagua mradi huo, Chongolo amesema sasa ameridhika na kazi nzuri ya usimamizi na utekelezaji unaoendelea.

"Nikupongeze sana Mkuu wa Wilaya na uongozi wa Halmashauri, leo mmefuta hasira zangu zote kwani nimeona na kufurahishwa na kazi nzuri ya usimamizi mliyoifanya katika mradi huu". Amesema Chongolo na kuongeza;

"Mara ya mwisho nilipokuja hapa nilikataa hata kusaini kitabu cha wageni, lakini sasa lazima mmefuta hasira zangu."

Hata hivyo, Mhe. Chongolo ameutaka Uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha ifikapo tarehe 25 Aprili 2025 bweni hilo liwe limeanza kutumika rasmi, huku akiahidi kushiriki chakula cha pamoja na Wanafunzi kama ishara ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Khatib Chaurembo, amesema tayari Halmashauri hiyo imefanya mabadiliko ya bajeti (realocation) kwa kutenga shilingi milioni 350 kwa ajili ya kukamilisha kazi zilizobaki.

Chaurembo amesema bwalo hilo linatarajiwa kugharimu shilingi milioni 800 hadi kukamilika kwake, na ameahidi kuwa mradi huo utakamilishwa kwa viwango na kwa muda uliopangwa.

Mhe. Chongolo amefanya ziara ya siku moja ya kutembelea Halmashauri hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Matukio katika Picha:

(Picha zote na Julius Evandino, TTC).

Matangazo

  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili January 24, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • DC Mwandobo Akutana, Wamiliki wa Maegesho

    April 16, 2025
  • Vyombo vya Ulinzi, Usalama Vyaimarisha Ushirikiano

    April 16, 2025
  • TAMISEMI Yaomba Trilioni 11.8 Bajeti ya 2025/2026

    April 16, 2025
  • Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Serikali Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi

    April 11, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa