• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

RC Songwe Afanya Ufuatiliaji Wanafunzi Kuripoti Shule

Imewekwa : January 8th, 2024

Na Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Fransis Michael leo tarehe 8 Januari 2024 amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Tunduma kwa lengo la kukagua zoezi la upokeaji wa Wanafunzi wa Awali, Darasa la Kwanza pamoja na Kidato cha Kwanza.

Dkt. Michael amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa alilolitoa hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa wote nchini.

Mkuu wa Mkoa huyo amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya upokeaji wa wanafunzi hao ambapo shule alizotembelea ni Shule ya Sekondari Tunduma TC, Shule ya Sekondari Uwanjani na Shule ya Sekondari Chipaka.

Katika ziara hiyo Dkt. Michael amekutana na walimu na wanafunzi ili kupata picha kamili ya jinsi upokeaji wa wanafunzi unavyofanyika lakini pia amefanya ukaguzi wa miundombinu ya shule na rasilimali zilizopo kama madawati.

Kupitia ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na hali ya kuripoti kwa wanafunzi shuleni kwani tayari wameshaanza masomo na amefafanua kuwa Shule ya Sekondari Chipaka imepokea Wanafunzi 38 kati ya wanafunzi 65 sawa na asilia 58.

Kwa upande wa Shule ya Sekondari Uwanjani wamepokelewa Wanafunzi 210 kati ya Wanafunzi 393 sawa na asilimia 53 huku Shule ya Sekondari ya Tunduma TC wameripoti Wanafunzi 92 kati ya Wanafunzi 103 sawa na asilimia 90 ya waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo.

Katika ziara hiyo, Dkt. Michael ametoa maelekezo kwa Maafisa Elimu na Walimu kuweka umuhimu wa kuwapa mapokezi bora Wanafunzi ili kuwawezesha kuanza masomo yao kwa ufanisi huku akiwasihi wazazi kuwapeleka shuleni watoto wote ambao wanastahili.

“Niwasihi wazazi wasiache kuwapeleka watoto shule kwa kuhofia kukosa sare sisi tumekwisha kutoa maelekezo kwa Walimu Wakuu wawapokee watoto hao huku wazazi wao wakiwa wanaendelea kuwatafutia sare hizo suala hili lisimkoseshe mtoto masomo ya awali” Amesema Dkt. Michael na kuongeza kuwa:

 “Mtoto anapoingia Kidato cha Kwanza au Darasa la Kwanza ni wakati muhumu sana kwake kuweza kuweka msingi wake wa elimu, masomo ya awali yakimpita anakuwa na msingi mbovu sana na ataanza kuichukia shule kwahiyo ndo maana tunasema mtoto apelekwe shule wazazi wataendelea kutafuta sare mtoto akiwa shule.”

Akifafanua kuhusu mikakati ambayo Mkoa imeweka ili kuhakikisha idadi ya wanafunzi wanaoanza shule inabaki hivyo mpaka wanapohitimu, Mkoa umeanzisha utaratibu wa kuboresha miundombinu ya baadhi ya Shule na kuweka mabweni ili kuzifanya kuwa shule maalum kwa ajili ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakikatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali wanaotoka.


Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa