• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

SERIKALI YATOA MTAMBO WA KUCHAKATA HEWA YA OXJENI HALMASHAURI YA TUNDUMA

Imewekwa : February 10th, 2023

Na William Maganga,Tunduma

Serikali imetoa kifaa cha kisasa cha kuzarisha hewa ya Oxjeni pamoja na mitungi 63 itakayo msaidia mgonjwa mwenye shida ya upumuaji sambamba na vifaa vya upasuaji na upimaji katika Halmashauri ya Mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe.

Akizungumza leo tarehe 10/2/2023 Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. Enock Mwambalaswa amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na  Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta vifaa hivyo na bado gharama yake haijatolewa kwani bado vifaa vingine vinaendelea kuja na kwamba kinu hicho cha kuzalisha hewa kitaweza kuhudumia wagonjwa wa ndani na nje ya Tunduma.

Alisema sambamba na hilo pia serikali imewapa vifaa vya Milioni 370 vikiwemo vya upasuaji hali nitakayoongeza utoaji wa huduma za matibabu na kumudu wingi wa watu hasa ukichukulia Tunduma ni Lango Kuu la nchi za SADC hali iliyopelekea kuwa na muingiliano mkubwa wa watu.

Dkt. Mwambalaswa alisema vifaa hivyo ni vya kisasa zaidi kama kifaa kinachoruhusu hewa ya Oxjeni kumfikia mgonjwa (Flow meter with humidifier), Kifaa cha kupimia umeme kwenye moyo (Electro cardiograph), Kifaa cha kubebeka cha mionzi laini (portable ultrasound), Kifaa cha kupimia macho (wall mounted ophthalmoscopes), na Kifaa cha mionzi mizito (X-Ray ).

 Alivitaja vifaa vingine kuwa ni Meza ya kubebea wagonjwa (stretchers), Mtambo wa kuchakata na kutunza hewa ya Oxjeni (PSA Oxygen generating plant),Vifaa anavyo vaa mtaalam kujikinga na mionzi (Protective gear for X-Ray), Vifaa vya kumuongezea mgonjwa hewa ya Oxjeni (ventilator) na vifaa mbalimbali vinavyosaidia wakati wa upumuaji (Endotracheal tubes).

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa, “Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa kupata matibabu salama kwa kuwapatia vifaa hivi, ni jukumu letu sasa wataalamu kuvitumia kwa weledi na uadilifu ili vidumu katika kuwatibu walengwa” alisisitiza Mkurugenzi Magesa

Aliongeza kuwa mbali na hilo “Serikali imetupatia fedha zinazotumika kujenga vituo vitano vya afya lengo ni kuhakikisha wananchi wa Mji wa Tunduma wanasogezewa huduma karibu huku Halmashauri kwa kutumia fedha za mapato ya ndani asilimia 70 tunazitumia kujenga miradi ya maendeleo” alisema Magesa

Tunduma ni lango kuu la nchi za kusini mwa Afrika (SADC) hivyo, kutokana na muingiliano mkubwa wa wananchi wanaoutumia mpaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameona aongeze nguvu kwenye sekta ya afya kuongeza uhakika wa matibabu kwa wananchi wa ndani na nje ya Tunduma

Kwa upande wa wananchi wa Mji wa Tunduma akiwemo Isakwisa Mwashilindi alisema wanakila sababu ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuwajali wananchi wake kwa kuleta vifaa vya aina hiyo na kwamba huduma za afya zimeboreshwa mara dufu ukilinganisha na ilivyokuwa awali.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa