• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Shechambo: Hakikisheni Kaya Zote Zina Vyoo

Imewekwa : February 22nd, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Watendaji wa Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Usafi wa Mazingira – CLTS katika Halmashauri ya Mji Tunduma wametakiwa kuhakikisha kuwa kila Kaya katika Halmashauri hiyo inakuwa na choo bora na kukitumia ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Afya wa Halmashauri hiyo, Pendo Shechambo alipikuwa akizungumza na viongozi hao kutoka katika Kata 7 za Halmashauri ya Mji Tunduma wakati wa kikao cha pamoja na Timu ya Maafisa Afya wa Halmashauri hiyo kilichofanyika kwa nyakati tofauti kwenye Ukumbi wa Shule ya Msingi Danida na Ukumbi wa Kituo cha Afya Tunduma tarehe 22 Februari 2024 kwa lengo la kuimarisha kampeni ya usafi wa mazingira.

Kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Msingi Danida kilijumuisha wajumbe kutoka Kata za Sogea, Maporomoko, Kaloleni na Tunduma huku kile kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Kituo cha Afya Tunduma kulijumuisha Wajumbe wa Kata za Muungano, Mwakakati na Makambini.

Shechambo amewaasa Wenyeviti na wajumbe wa Kamati ya CLTS kuhakikisha kuwa hakuna kaya au taasisi ambayo inakosa choo safi na salama na kuhamasisha Wananchi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama vile Kipindupindu, majonjwa ya matumbo, Ugonjwa wa Jicho Jekundu na UVIKO 19.

“Magonjwa yote ya mlipuko yanayotokea kipindi hiki ni magonjwa yanayotokana na uchafu…tukiweza kuhamasisha jamii yetu vizuri wakafahamu umuhimu wa kutumia choo safi na kusafisha mazingira yao tutaweza kuepuka magonjwa haya.” Alisema Shechambo na kuongeza;

“Mtu akiumwa typhod au kipindupindu tafsiri yake ni kuwa mtu huyo amekula kinyesi…usione fahari kuumwa magonjwa hayo maana yake ni kuwa wewe ni mchafu tuchemshe maji ya kunywa na kuyachuja vizuri kabla ya kunywa.”

Naye,  Afisa Afya, Bakari Ibrahim amebainisha sifa za Choo bora ni kile chenye sakafu inayosafishika, kiwe na paa, kiwe na kuta imara, kiwe na mlango unaofunga ndani na njee, kiwe na maji ya kutawazia kwa ndani na kiwe na maji tiririka na sabuni kwa ajili ya kunawa mikono kwa nje.

“Tunafanya kampeni ya kukagua vyoo ili kuona ubora wa vyoo tulivyonavyo maana ili kupambana na magonjwa ya mlipuko ni lazima kuwa na vyoo bora na siyo bora choo tu.” Alisema Ibrahim na kuongeza;

“Wakati tunaweka mazingira mazuri ya vyoo kwenye kaya tuzingatie na taasisi zetu kama shule, ofisi za watendaji, makanisa na misikiti kuwa na vyoo bora”.

Mwaka 2012 hadi 2013 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau ilianzisha kampeni ya kitaifa iitwayo Kampeni ya Usafi wa Mazingira (National Sanitation Campaign) ambayo ilikuwa na lengo la kupunguza jamii za watu ambao hawatumii vyoo bora.

Vilevile, mpaka kufika mwaka 2030 Tanzania kama nchi nyingine ulimwenguni inatakiwa kuhakikisha kuwa hakuna kaya ambayo haipati maji safi na salama pamoja na kuwa na mazingira safi hii ni kwa mujibu wa Lengo Namba 6 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya mwaka 2015 ambayo Tanzania ilisaini mkataba wake.

Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa