• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

SHIRIKA LA RESTLESS DEVELOPMENT TANZANIA LATOA ELIMU TUNDUMA

Imewekwa : September 2nd, 2022

Shirika la Restless Tanzania lenye kazi ya Kushauri, Kulea na Kuunganisha maelfu ya vijana kuongoza mabadiliko ya vijana nchini Tanzania kupitia Mradi wake wa “Kijana Wajibika” limefika katika Halmashauri ya Mji Tunduma, Wilayani Momba kwa lengo la kuelimisha jamii hususani vijana kuhusiana na kazi mbalimbali  zinazofanywa na shirika hilo kama uongozi kwa vijana, kutokomeza tatizo la ukeketaji kwa wanawake, kutokomeza ukatili wa kijinsia, Stadi za Maisha na ujasiliamali.

Wakati wa utoaji wa elimu hii Shirika hili kupitia vijana wa wajibikaji limetumia muda huo kuzungukia maeneo mbalimbali kama Shule za Msingi na sekondari, Vituo vya afya na Zahanati, Vikundi vya wanawake ambalo ndilo kundi kubwa linalokumbwa na tatizo la ukatili  wa kijinsia sambamba matatizo ya afya ya uzazi.

Mojawapo ya kazi zilizoelezwa na shirika hili ni Pamoja na utoaji wa elimu dhidi ya ukeketaji ambapo Wanawake na Watoto wa kike wengi ambao hawajasoma ndio wanaonyanyasika dhidi utamaduni huu wa ukeketaji kwani huonekana kutokuwa na mchango wa kiuchumi katika jamii zao hivyo huishi Maisha ya kimaskini na kuendelea kunyanyasika.

“ Tabia hii imekuwa ikirithiwa kutoka kizazi hadi kizazi huku ikitumiwa kama njia ya kuandaa Watoto wa kike kuelekea utu uzima kitendo ambacho si sahihi kinatakiwa kutokomezwa kwani madhara yatokanayo na ukeketaji ni makubwa na ya muda mrefu. “

Aidha ,Shirika hili limemulika tatizo kubwa la Ukatili wa kijinsia na kuitaka jamii kutofumbia macho matukio yanafanana na tukio hili kwani vitendo vya kikatili vinatokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika ngazi ya kaya, mahali pa kazi, maeneo ya biashara kama masoko,mashuleni na mahali pengine katika jamii zetu.

 Hivyo ili kufanikisha usawa wa kijinsia kwa jamii ya watanzania Serikali kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali  kama Restless imeendelea kuimarisha ujenzi wa vituo vya kijamii vya malezi , makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto, imeanzisha madawati  ya jinsia na Watoto katika vituo vya polisi ili wanajamii waweze kuripoti vitendo  vya ukatili vinavyofanyika katika jamii zao.

Kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo vijana na wanawake wengi kuhusiana na afya ya uzazi Pamoja na makuzi Shirika la Restless limetoa elimu hii ili kuzuia matatizo au madhara yanayosababishwa na kukosa elimu ya uzazi kama mimba za utotoni, magonjwa , utoaji mimba na hata kifo ,lengo la elimu hii ni kumlinda mtoto na kumuwezesha kusoma  kwa maendeleo mazuri ya baadaye na kwa manufaa taifa kwa ujumla.

Kwa kuwa Tunduma ni mji unaojishughulisha na biashara mbalimbali Shirika la Restless liliona kuna haja ya kutoa elimu kwa vijana juu ya stadi za Maisha na ujasiliamali ili kuwezesha kundi hili kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika mji huu kuliko kusubiri nafasi za ajira zinazotolewa na serikali hivyo kuwataka vijana kujiajiri wenyewe kwa kuzingatia  matumizi sahihi ya fedha na kuunda vikundi mbalimbali ya ushirika ili kuwezeshana.

Sambamba na hilo wametoa elimu ya uraia na ushirikishwaji kwa vijana katika mipango mbalimbali ya kimaendeleo inayopangwa katika ngazi za familia na Serikali kwani kundi la vijana ndilo linalotegemewa kuliinua taifa lolote katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa