• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

Imewekwa : March 13th, 2023

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema utunzaji siri za Serikali ni jambo muhimu huku akiwataka Wakuu wa Wilaya kuacha kutumiana nyaraka za Serikali kwa kutumia mitandao ya kijamii au barua pepe binafsi.


Akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara leo Machi 13, 2023 kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi hao kuwachukulia hatua watumishi wazembe, wabadhirifu na wanaokwamisha miradi ya Serikali katika maeneo yao.


“Utunzaji siri za Serikali ni muhimu sana hususani katika kipindi hiki cha utandawazi na matumizi ya mitandao ya kijamii yawapasa mzingatie kuwa siri ndio uhai wa Serikali. Hivyo, ni lazima kudhibiti uvujaji wa siri za Serikali. Epukeni kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama whatsapp, ama email binafsi kutuma nyaraka za Serikali’ amesitiza Dkt. Mpango.


Amewataka watoa mada kuhakikisha wanasisitiza kuhusu matumizi ya walinzi binafsi (bodyguards) na Waandishi wa Habari binafsi katika Ofisi za Umma kwa kuwa zipo taratibu za umma za kupatiwa wasaidizi hao.



Dkt. Mpango amewataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia maadili, nidhamu na uwajibikaji wa watumishi kwa wananchi na kuepuka lugha za matusi na kujifanya miungu watu.


“Msiende kuwa Miungu watu, nendeni mkatende haki kwa wananchi na watumishi walio chini yenu. Wahudumieni wananchi kwa staha, sikilizeni kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati. Ninyi kama Viongozi mnapaswa kuongoza kwa mfano na kuweni makini wakati wote mnapozungumza na Umma, hakikisheni mnatumia lugha fasaha na nzuri.”amesema .

“Epukeni kutoa lugha ya matusi. Aidha, mienendo yenu na muonekano wenu mbele ya jamii uwe ni wa mfano, mienendo isiyofaa kama ulevi, ufuska, unyanyasaji wa kijinsia, matumizi mabaya ya madaraka yenu, ufisadi, rushwa n.k. haiendani kabisa na dhamana au heshima ya Mkuu wa Wilaya.”


Aidha, amesema kuwa Mkuu wa Wilaya anayetarajiwa na Serikali ni yule anayetenda haki, mwaminifu/mnyoofu, mwadilifu, mwenye tabia njema na mchapakazi.

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa