• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

Imewekwa : March 11th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Momba MHE. Fack Lulandala ameyasema hayo wakati akikabidhi pikipiki 21 zenye thamani ya Tsh. 63,000,000/= kwa Ma Afisa Ugani 21 wa Halmashauri ya Mji Tunduma

Mhe. Lulandala amewaeleza ma afisa Kilimo hao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezitoa pikipiki hizo ziwasaidie katika kutekeleza majukumu yao ya kilimo ili taifa liwe na kilimo chenye tija.

“Nijukumu lenu kuzitunza pikipiki hizi kwani serikali imetumia gharama kubwa sana katika ununuzi wake sasa sitegemei kusikia Afisa Ugani umeenda nayo kulewa bar hapo hatutaelewana” alisema Dc Lulandala

Mhe. Lulandala amesema kuwa Rais ameona kuwa nchi hii haiwezi kuwa na kilimo bora na chenye tija ikiwa maafisa ugani hawajasidiwa kupata vyombo vya usafiri na kuweza kuwafikia wakulima shambani kwa maana ya kuwapatia elimu

“Ahadi hii ya kuwanunulia pikipiki aliitoa yeye mwenye Rais katika mkutano na maafisa ugani nchi nzima mliohudhuria wote waka 2022 pale Jijini Dodoma na leo Mhe. Rais ametekeleza kwa vitendo ahadi yake” alisisitiza Mhe. Lulandala

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Philemon Magesa aliwapongeza maafisa ugani wote kwa kupata pikipiki toka kwa Rais na kuwaasa kuzitumia vizuri kwa lengo la kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima wa Tunduma

“Mkumbuke kuwa pikipiki hizi baada ya miaka miwili zitakuwa za kwenu jumla hivyo jitahidini kuzitunza kwa weledi na kuzitumia kwa matarajio ya serikali ili kuinua uchumi wa wakulima wa Tunduma na Taifa kwa ujumla” alisema Mkurugenzi Mgesa

Aidha Mkurugenzi Magesa aliwaambia maafisa ugani wanaokabidhiwa pikipiki hizo juu ya matumizi bora

“Sitaki kusikia pikipiki hizi mmezigeuza kuwa Bodaboda mnafanyia biashara ya kubeba abilia, hatua za kinidhamu lazima zichukuliwe sita muonea haya Afisa ugani yeyote ambaye ataenda kinyume na matakwa ya matumizi ya vifaa hivi” alisisitiza Mkurugenzi Magesa

Aidha Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi bwana Lusajo Mwalukasa amewataka ma afisa ugani wote kujua kuwa pikipiki walizopewa ni kwa ajili ya kuwatembelea wakulima na kutoa elimu

“Matumaini yangu kuwa kila Mkulima sasa tutamfikia na kumpimia udongo wake na tuwashauri juu ya matumizi ya mbolea na viwatilifu vingine, mashine ya kupimia udongo tunayo na tunapima bure kabisa, zamani iliwalazimu wakulima kuleta Udongo Halmashauri ili wapimiwe kwa pikipiki hizi tutawafuata hukohuko mashambani” alisisitiza Mwalukasa

Halmshauri ya Mji Tunduma imepata pikipiki 21 zenye thamani yaTsh. 3,000,000/= kwa kila moja na kufanya jumla ya thamani yake kuwa Tsh. 63,000,000/= Lengo kuu ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa