• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TAASISI ZA UMMA ZAPATA MGAO WA BIDHAA ZA MAGENDO MPAKA WA TUNDUMA

Imewekwa : February 9th, 2023

Na William Maganga,Tunduma

MKUU wa mkoa wa Songwe Wazir Kindamba ameongoza zoezi la ugawaji wa bidhaa zenye thamani ya Tsh. 12,433,920/= zilizokamatwa zikiingia nchini kwa njia za magendo kupitia mpaka wa Tunduma zikitokea nchi za jirani huku akiwapa changamoto maafisa wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuzidisha operesheni.

Mhe. Kindamba alisema katika operesheni iliyofanyika takribani siku kadhaa mamlaka ya mapato kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamefanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikivushwa kwa njia za panya kuingia nchini huku wahusika wakishindwa kuzilipia.

Alisema baada ya wenye mizigo hiyo kushindwa kuilipia, wamekutana na kuzigawa kwa makundi maalum iwemo taasisi za serikali na kusema mamlaka ya mapato (TRA) kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wote kuhakikisha wanafuata utaratibu uliopo wa kuingiza bidhaa hizo nchini.

Kaimu Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Songwe, Valelian Thadei alisema katika operesheni za mara kwa mara zilizofanywa kwa kushirikiana na meneja wa forodha Tunduma Mohammed Shamte na jeshi la polisi walifanikiwa kukamata bidhaa hizo zenye thamani ya Tsh. 12,433,920/=

 Alisema bidhaa hizo ambazo ni Sukari kilo 3,420 thamani yake ni Tsh. 10,260.000, Biskuti katon 96 thamani yake ni Tsh. 1,453,920 na Juisi Apple katon 15 thamani yake ni Tsh.720,000 jumla yake ni Tsh.12,433,920.

Miongoni mwa Taasisi zilizopata mgao ni shule za sekondari za Tunduma, Songwe, Vwawa, Mlangali, Simbega, Tunduma Tc, Mwl. J. K. Nyerere, Mpemba, Kafule, Chikanamilo, Maweni, Kanga pamoja na shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Tunduma na shule ya msingi Mwenge.

Valelian aliongeza kuwa pia wamegawa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mbozi Misheni, Jeshi la Magereza, kituo cha UMISETA na UMITASHUNTA ambapo tayari wahusika wamezipokea huku akimuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa zoezi la operesheni litaendelea ili kuhakikisha hakuna mtu anayevusha magendo.

Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Tunduma Bi. Patricia Mbigili alisema anashukuru sana kwa mgao wa vifaa hivyo kwani vitasaidia katika matumizi ya wanafunzi wa shule za bweni na kupongeza sana busara za kuamua kuvigawa kwa taasisi za umma

Mpaka wa Tunduma unatumika na nchi wanachama za kusini mwa Afrika (SADC) na kumekuwepo na muingiliano mkubwa wa watu wanaofika kufanya biashara huku wengi wao wakiwa si waaminifu wakitumia njia za panya kuvusha bidhaa na kuikosesha serikali mapato, ipo haja mamlaka husika kuongeza kasi ya kuwadhibiti.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa