• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TAMISEMI Yaomba Trilioni 11.8 Bajeti ya 2025/2026

Imewekwa : April 16th, 2025

OR - TAMISEMI

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  imewasilisha bungeni makadirio ya mapato kwa mwaka 2025/26 yenye takribani Shilingi trilioni 11. 783 kwa ajili ya wizara na taasisi zilizo chini yake.

Bajeti hiyo imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 10.125  zilizotengwa mwaka 2024/25 hadi kufikia Shilingi trilioni 11.783 na kuwa na ongezeko la  zaidi ya Sh trilioni 1.66.

 Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema shilingi trilioni 3.95 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi trilioni 2.5 ni fedha za ndani, ikijumuisha Shilingi bilioni 613.44 za mapato ya ndani ya halmashauri na Shilingi trilioni 1.45 ni fedha za nje.

Pia, amesema Shilingi trilioni 7.84 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara Shilingi trilioni 6.3 na matumizi mengineyo Shilingi trilioni 1.53 ikijumuisha Shilingi trilioni 1. 067 za mapato ya ndani ya halmashauri.

“Tumewasilisha si tu makadirio ya mapato na matumizi, bali tumeweka mbele yetu dira ya matumaini, ramani ya maendeleo na ahadi ya uongozi unaowajibika. TAMISEMI haitafuti sifa ya kisiasa, tunatafuta suluhisho sahihi kwa maisha ya mtanzania wa kawaida.”

Aidha, Mchengerwa ametoa wito kwa mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na wananchi wote kushirikiana, kusonga mbele kwa mshikamano.

“Kwa dhamira hii, na kwa imani kubwa katika maono ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunawasilisha bajeti hii kama zana ya kazi, dira ya matumaini na silaha ya mapinduzi ya kiutawala, kiuchumi na kijamii.”

“Kwa hiyo, tunasema kwa ujasiri mkubwa, TAMISEMI, ndiyo msingi wa maendeleo endelevu. Kila Shilingi ina Jukumu, Kila Kiongozi ana Wajibu na Kila Mwananchi ana Nafasi!”

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, vyama vya siasa na Serikali kesho tarehe 12 Aprili, 2025 wanatarajiwa kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zitakayotumika kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu (2025).

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari mkoani Dodoma leo tarehe 11 Aprili, 2025 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhan amesema chama cha siasa ambacho hakitasaini maadili hayo hakitaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Kailima amesema maadili hayo yameandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 162 (1), (2) na (3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 ambacho kinaitaka Tume baada ya kushauriana na vyama vyote vya siasa na Serikali, kuandaa na kuchapisha katika Gazeti la Serikali Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zitakazoainisha maadili ya vyama vya siasa, Serikali na Tume wakati wa kampeni za uchaguzi na uchaguzi na utaratibu wa utekelezaji wake.

Amesema kifungu hicho kinaelekeza kuwa kanuni za maadili zitasainiwa na kila chama cha siasa, kila mgombea kabla hajawasilisha fomu ya uteuzi, Serikali na Tume na zitapaswa kuzingatiwa na wahusika wote waliosaini.

Ameongeza kuwa tayari maandalizi yote muhimu yameshafanyika na mawasiliano yameshafanyika baina ya Tume, Serikali na vyama vya siasa na kwamba kinachosubiriwa ni kuwasili kwa wahusika jijini Dodoma kwa ajili ya kusaini kanuni hizo za maadili kesho.

Amefafanua kuwa zoezi hilo litafanyika kwa siku moja tu na kwamba baada ya hapo chama ambacho hakijasaini kanuni hizo za maadili hakitapata fursa ya kusimamisha wagombea.

Katika hatua nyingine, Kailima amesema Tume inaendelea vizuri na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba tayari imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kwamba maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwa awamu ya pili yanaendelea ambapo Tume inatarajiwa kutangaza ratiba ya zoezi hilo hivi karibuni.

Matukio katika Picha:

(Habari na Picha zote kwa Hisani ya OR - TAMISEMI).


Matangazo

  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili January 24, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • DC Mwandobo Akutana, Wamiliki wa Maegesho

    April 16, 2025
  • Vyombo vya Ulinzi, Usalama Vyaimarisha Ushirikiano

    April 16, 2025
  • TAMISEMI Yaomba Trilioni 11.8 Bajeti ya 2025/2026

    April 16, 2025
  • Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Serikali Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi

    April 11, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa