• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Tanduma Yanufaika na Msaada Uliotolewa na Benki ya NMB Mkoa wa Songwe

Imewekwa : November 3rd, 2023

Mkuu wa Mkoa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael ameishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 56 ikiwemo mabati 440 na madawati 491 ikiwa ni mchango wa Benki hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

 Dkt. Michael ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe tarehe 03 Novemba 2023.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema msaada huo utasaidia kuboresha mazingira ya Wanafunzi kujisomea huku akiwaahidi Wanafunzi wa Kidato cha Nne 2023 ambao wanatarajia kuanza mitihani tarehe 13 Novemba 2023 katika Mkoa wa Songwe kujitahidi kufanya vizuri na wote watakaopata Daraja la Kwanza atawachinjia ng’ombe na kula nao chakula cha mchana.

Dkt. Michael amepokea msaada huo na kusema utazinufaisha shule nane (8) za Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ambapo ameishukuru Benki hiyo kwa kuendelea kuwa karibu na Wananchi kwani msaada huo ni kielelezo tosha.


“NMB kwa kweli usemi huu wa ‘NMB, Karibu Yako’ ni kweli mpo karibu ya watu, kwa sababu mimi ninapofanya kazi zangu za kutembea kwa Wananchi vijijini napita sehemu ambazo siwezi kuamini naikuta NMB ipo hongereni sana, lakini zaidi ya hayo ni kwa yale mnayoyafanya kwa sababu ya maendeleo ya Wananchi kwa ujumla.” Anasema Dkt. Michael na kuongeza;

“NBM sehemu zote ambazo zina shughuli za kitaifa na ninyi mpo, na hili suala la Cooperate Social Responsibility mnalifanya kwa kiwango kikubwa sana na nimefurahi kwa sababu shilingi milioni 56.36 siyo fedha ndogo na mmeweza kutoa kwa shule nane (8) hizi ni fedha nyingi...ili kusudi watoto wetu hawa wapate mazingira mazuri ya kusomea, kama mtoto hapati mazingira mazuri ya kusoma hawezi pia kupata elimu inavyopaswa.”

Pia, Dkt. Michael ameipongeza Benki hiyo kwa kusimamia utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti zaidi ya milioni moja na kuisimamia matunzo yake.

“Hongereni sana NMB muendelee na moy huo sisi kama Serikali tupo pamoja na ninyi, kwa sababu sisi ndo wateja wenu…endeleeni kutoa huduma bora kwa Wananchi.” Amesema Dkt. Michael.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Chilongola amesema Benki hiyo inathamini jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo hivyo imekuwa na utaratibu wa kuchangia kama Mdau kwa kutambua jamii inayonufaika ndio Wateja wa Benki hiyo ambayo ina matawi katika Wilaya zote nchini huku akiushukuru uongozi wa Mkoa huo kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Benki hiyo.

“Pamoja na makubwa yanayofanywa na Serikali, sisi kama wadau tunao wajibu mkubwa wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii zetu kwani jamii hizi ndiyo zimeifanya Benki ya NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini.” Amesema Chilongola.

Chilongola amesema kwa miaka kadhaa sasa, NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu (madawati na vifaa vya kuezeka), afya (vitanda, magodoro yake na vifaa vingine vya kusaidia matibabu) na kusaidia majanga mbalimbali nchini.

Amesema NMB inatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wao wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni wao.

Chilongola ameongeza kuwa Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yake kwa jamii na ni kwa zaidi ya miaka saba mfululizo Benki hiyo imekuwa ikitenga asilimia moja (1) ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayowanzunguka.

Kiongozi huyo anayesimamia Benki ya NMB Nyanda za Juu inayojumuisha mikoa mitano ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa, ndiyo benki inayoongoza nchini huku ikiwa na matawi 228, mashine za ATM zaidi ya 700 nchi nzima, NMB Wakala ni zaidi ya 17,000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 5 idadi ambayo ni hazina kubwa ukilinganisha na benki nyingine nchini.


Matukio Katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa