• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TASAF IMETENDA MIUJIZA TUNDUMA

Imewekwa : June 7th, 2022

Mkazi wa Mtaa wa Chipaka kata ya Chipaka Bi. Anna Sichimata ameushangaza Umma wa Wanatunduma na Watanzania kwa ujumla baada ya kuonyesha mafanikio aliyoyapata tangu alipoanza kupokea Pesa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Julai mwaka 2015 hadi sasa 2022

Bi. Anna amesema kabla ya kuingia katika mpango wa TASAF maisha yake yalikuwa duni lakini baada ya mpango huo ameweza kujenga nyumba ya bati (SAUZI), analima mashamba na kununua Mbolea bila shida na kilimo chake kimekuwa kikikuwa mwaka hadi mwaka

"Wakati mkutano wa Mtaa umeitishwa ili kuwapata walengwa wa TASAF nilionekana mimi pia ni mmoja wapo wa walengwa ila niliona kama udhalilishaji kutokana na hali yangu ya umasikini, nashukuru mtendaji wa Mtaa kwa kunielewesha kuhusu mpango huu, hadi sasa mafanikio niliyo nayo yametokana na mpango wa TASAF", amesema Bi. Anna.

Bi. Anna ameeleza kuwa kabla ya TASAF alikuwa akiishi kwenye nyumba yenye makazi duni ambayo waliyo ijenga marehemu wazazi wake zamani sana. Lakini sasa ameweza kununua kiwanja na kujenga nyumba ya bati ambayo inamfanya kila siku amuombee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani Pesa hizi anazozitoa Rais zinawafikia walengwa moja kwa moja.

Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Mji Tunduma Bwana Freza Mapunda wakati akiongea na wanufaika kabla ya zoezi la utoaji Pesa kuanza aliwaasa wanufaika kuwa lengo la mfuko wa TASAF ni kumsaidia mnufaika apige hatua haraka kutoka kwenye umasikini na aweze kuyamudu maisha ya kaya yake kwa kuwa na uhakika wa chakula, huduma za fya na elimu na hata kuchangia katika pato la Taifa kwa kuzalisha mali kupitia kilimo, ufugaji na biashara, nawashauri wanufaika wote mzitumie pesa hizi vizuri ili ziweze kuleta matokeo chanya katika kuinua kaya zenu

Katika dirisha hili la TASAF la Mwezi Mai Halmashauri ya Mji wa Tunduma umetoa jumla ya Tsh. 66,340,000/= kwa wanufaika 1677 wanaopatikana ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa