• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TMA YAKUTANA NA SEKTA MBALAMBALI NCHINI ILI KUJIPANGA NA MSIMU WA MASIKA 2023

Imewekwa : February 23rd, 2023

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na msimu wa masika, katika Ukumbi wa NIT, jijini Dar es salaam, tarehe 20 Februari, 2023.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi, alisema lengo la mkutano huo ni kujadili mwenendo wa mvua za msimu wa Masika 2023 na kuandaa taarifa zinazolenga kuchochea matumizi sahihi za huduma za hali ya hewa kulingana na utabiri utakaotolewa. Aidha, alisisitiza kuwa ushirikiano na ushirikishwaji wa wadau ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

“Tunapoelekea kutoa utabiri wa mvua za Masika (Machi hadi Mei), 2023 ninapenda kuipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali kutoa michango yao katika shughuli za utoaji wa huduma za hali ya hewa ambazo ni pamoja na mchakato wa utabiri wa misimu ya mvua. Ushirikiano na ushirikishwaji huu ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambapo dunia pamoja na nchi yetu tunakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa”. Alisema Dkt. Nyenzi.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua thabiti za kukabiliana na hali hii kwa kuimarisha miundo mbinu ya Hali ya Hewa ikiwemo ununuzi wa vifaa kama vile vifaa vya kisasa vinavyojiendesha vyenyewe na Rada”. Alisisitiza Dkt. Nyenzi.

Awali wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TMA, Dkt.Ladislaus Chang’a aliishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kuendelea na uwekezaji katika miundombinu ya hali ya hewa hapa nchini, kupitia jitihada hizo, Mamlaka imeendelea kutoa taarifa za utabiri wa maeneo madogo madogo kwa wilaya zote za mikoa iliyopo katika ukanda unaopata mvua za Masika na hivyo kusaidia katika kufanya maamuzi stahiki kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi, na pia kupunguza madhara ya hali mbaya ya hewa inapojitokeza.

“Kama mnavyotambua, mvua za Masika ni mahsusi kwa maeneo ya pwani ya kaskazini, nyanda za juu kaskazini mashariki, na Ziwa Viktoria ambayo hupata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Masika na Vuli). Mvua hizi zina mchango mkubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, nishati, maji n.k. Hivyo, taarifa sahihi za hali ya hewa pamoja na athari zake ni muhimu kupatikana kwa wakati ili kuwezesha jamii na wadau kujipanga na kuandaa shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao”. Alisema Dkt. Chang’a.

Kwa upande wake Bi,Wilfrida Ngowi Mratibu Kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu alisema ‘’Serikali imeweka na imeendele kuimarisha mifumo na taratibu ya kukabiliana na maafa yatokanayo na matukio ya Hali mbaya ya Hewa ikiwemo mafuriko.

Naye,James Kirahuka Mhandisi Rasilimali Maji, akiwasilisha mrejesho wa msimu wa mvua uliopita, alisema baada ya kupokea utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa mvua za Vuli 2022 ukionesha upungufu wa mvua, TANESCO ilijipanga kwa kuongeza njia zingine za uzalishaji wa umeme ili kupunguza makali ya changamoto ya upatikanaji wa umeme.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, inatarajia kutoa rasmi taarifa ya msimu wa mvua za Masika tarehe 23 Februari 2023.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa