• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TRILIONI 2.7 ZA TASAF ZILIZOTOLEWA NA MHE. RAIS ZITUMIKE KUWASAIDIA WAZEE, WANAWAKE, WATU WENYEULEMAVU NA VIJANA TUNDUMA

Imewekwa : January 21st, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka waratibu wa TASAF kuhakikisha trilioni 2.2 zilizotolewewa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Kuzinusuru Kaya Maskini zinatumika ipasavyo kuboresha maisha ya wazee, wanawake, watu wenye ulemavu na vijana walio katika kaya hizo.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo alipokuwa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa ziara ya Siku moja tarehe 20-01-2022 kuwa anatamani kuona walengwa wa TASAF wanasimamiwa vizuri ili wawe na vikundi vya ujasiriliamali ambavyo vitapata mkopo wa asilimia 10 katika Halmashauri na kutumia mikopo hiyo na ruzuku wanayoipata kunyanyua maisha yao kiuchumi.

“Walengwa wa TASAF wakiwemo wazee, wanawake, watu wenye ulemavu na vijana wakiunda vikundi na kujishughulisha na ujasiriamali watakuwa kwenye mazingira mazuri ya kujikwamua kutoka katika hali duni waliyonayo,” Mhe. Ndejembi amefafanua.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka waratibu wa TASAF kuhakikisha wanashirikiana na wataalam wa Idara za kilimo, mifugo na maendeleo ya jamii kuwatembelea walengwa wa TASAF mara kwa mara ili kuwapatia ujuzi na utaalamu utakaowasaidia kuwa na vikundi bora vitakavyowawezesha kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Tunduma anlieleza kuwa, Halmashauri ilianza kutekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF, February 2020 ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa TASAF awamu ya tatu kwa Kipindi cha pili. Katika awamu hiyo TASAF imeweza kufikia jumla ya mitaa 71 katika kata zote 15 za Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mitaa hiyo imefikiwa kwa awamu mbili tofauti ambapo mitaa 57 ilifikiwa na mpango wakati Tunduma ikiwa kama kijiji katika Halmashauri ya wilaya ya Momba na mitaa 14 imefikiwa katika kipindi cha pili cha utekelezaji. Kwa kufuata taratibu na vigezo vya  utambuzi na uandikishaji wa kaya maskini sana jumla ya kaya 1698 zimekidhi vigezo  na kupokea ruzuku iliwemo mitaa 14 ambayo imepokea ruzuku kwa kipindi kimoja cha mwezi September – October 2021.

Dhumuni la mpango ni kuziwezesha Kaya Maskini kuongeza kipato na fursa za kuboresha upatikanaji wa mahitaji muhimu. Mpango huo umebuniwa kwa kuzingatia umuhimu wa uimarishaji rasilimali watu kwa kaya lengwa zilizochaguliwa kwa vigezo vilivyowekwa na kuzingatia masuala yanayohusiana na Afya, Lishe na Elimu. Lengo kuu la Mpango ni kuzipatia ruzuku Kaya za walengwa ili kumudu mahitaji ya msingi, kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na kujiongezea kipato na hatimaye kutoka katika hali ya umaskini sana.

Bwana Magesa alieleza, Utimizaji wa masharti Elimu na Afya Jumla ya watoto 1,077wamenufaika na ruzuku ilitolewa kwa kutimiza masharti ya elimu na afya. Watoto1,018  wa shule za msingi  na sekondari walipata ruzuku ya sh. 2000 - 6000 kwa mwezi kwa kila mtoto. Watoto  59 chini ya miaka  (0-5)  walinufaika  na  ruzuku ya sh.5000 kwa  mwezi kwa kila mtoto. Ruzuku hizo huongeza kipato katika kaya na pia kununua mahitaji muhimu ya watoto ikiwepo uniform, daftari, chakula, madawa na michango midodgomidogo endapo itatokea ambapo awali ilikuwa vigumu kutimiza huduma hizo katika kaya.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa