• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUNDUMA KINARA HOJA ZA CAG MKOA WA SONGWE YAPATA HATI INAYORIDHISHA MIAKA SITA MFULULIZO

Imewekwa : June 24th, 2022

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali Bi. Chausiku Mluge ameyasema hayo wakati akitoa taarifa katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji Tunduma la kujadili Hoja za CAG za mwaka wa fedha 2020/2021

Bi. Mluge alieleza kuwa, Hati ya ukaguzi ni maoni ya mkaguzi yanayoeleza kama taarifa za fedha zilizokaguliwa zimetayarishwa kwa kuzingatia viwango vya taaluma ya uhasibu na mambo yote muhimu, kwa mujibu wa misingi inayotumika katika uandaaji wa taarifa hizo. Hati ya ukaguzi pia inazungumzia kama taarifa za fedha zilizowasilishwa zina maelezo ya kutosha katika kuelezea vizuri na kwa upana zaidi taarifa hizo ili ziweze kueleweka kwa watumiaji.

Kuna aina Nne za hati ambazo ni Hati inayoridhisha, Hati yenye Shaka, Hati mbaya na kushindwa kutoa maoni.

Katika Mwaka wa Fedha 2020/21 Halmashauri ya Mji Tunduma ilipata Hati inayoridhisha (Unqualified Opinion). Hii ikiwa ni kwa Mwaka wa 6 mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2020/2021. Hati ya aina hii inatolewa wakati

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amejiridhisha kuwa, kutokana na ushahidi uliokusanywa wakati wa ukaguzi, Halmashauri imeandaa taarifa za fedha kwa usahihi na kwa kuzingatia vigezo vyote vinavyotumika vya uandaaji wa taarifa za fedha, yaani Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Taarifa za Fedha katika Sekta ya Umma pamoja na miongozo mingine.

Aidha, katika ukaguzi wa shughuli za Mradi wa Mfuko wa Afya wa Pamoja (HSBF) Pamoja na shughuli za manunuzi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliweza kutoa hati ya ukaguzi inayoridhisha.

Katika Taarifa ya CAG ametoa aya yenye masuala ya mkazo ili kutoa angalizo kwa watumiaji wa taarifa za fedha, masuala hayo aliyachukuliwa kuwa muhimu sana kwa watumiaji wa taarifa hizo kuyafahamu ili waweze kuzielewa vizuri zaidi taarifa za fedha zilizokaguliwa.

Katika mwaka wa fedha 2020/2021 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali alitoa jumla ya mapendekezo 33,

Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Tunduma ilipokea mapendekezo hayo ya Ukaguzi na kuyafanyia kazi kikamilifu na mnamo tarehe 09.05.2022 Halmashauri iliwasilisha utekelezaji wa mapendekezo ya Mkaguzi katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Baada ya uhakiki kati ya mapendekezo 33 yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Jumla ya mapendekezo 16 sawa na asilimia 48.4 yametekelezwa kikamilifu na kufungwa na mapendekezo 17 sawa na asilimia 51.6 yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji (Under Implementation) ambapo Mkaguzi atayapitia wakati wa ukaguzi wa mwaka wa fedha 2021/22 kwa ajili ya kujiridhisha kama uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu umeboreshwa.

Aidha, kwa upande wa ukaguzi wa Mfuko wa afya wa pamoja (HSBF) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali alitoa Jumla ya mapendekezo 6 kati ya mapendekezo hayo mapendekezo 3 yamefanyiwa kazi kikamilifu na kufungwa, Pendekezo 1 bado halina utekelezaji na Mapendekezo 2 yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji (Under Implementation) ambapo Mkaguzi atayapitia wakati wa ukaguzi wa mwaka wa fedha 2021/22 kwa ajili ya kujiridhisha kama kuna uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu ili mapendekezo hayo yaweze kufungwa.

Menejimenti ya Halmashauri inaendelea kupitia na kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani kwa kuhakikisha kuwa mifumo iliyopo inafanya kazi vizuri katika kupunguza au kuondoa dosari ambazo zinaweza kusababisha hoja za kiukaguzi. Aidha, Mafunzo ya mara kwa mara yanaendelea kutolewa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi katika masuala ya uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu.

Mwisho, Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali alimpongeza mwenyekiti wa Halmashauri, wajumbe wote wa Baraza la Madiwani kwa kazi nzuri iliyowezesha Halmashauri kupata hati inayoridhisha (Unqualified opinion). Hii ni kiashiria kuwa Kamati ya fedha inatimiza majukumu yake kikamilifu kwa kutoa mwongozo wa mchakato wa kuandaa taarifa za fedha, mchakato wa ukaguzi, Kufanya mapitio ya mfumo wa udhibiti wa ndani wa Halmashauri na utii wa sheria, kanuni na taratibu.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa