• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUNDUMA YAJENGA KITUO CHA AFYA CHA MFANO KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Imewekwa : January 23rd, 2023

Na William Maganga Tunduma:

Baada ya juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha huduma za Afya kwa kujenga vituo vya Nchi nzima, Halmashauri ya Mji Tunduma imeamua kujenga Kituo cha Afya Chapwa kwa Fedha za mapato ya ndani ili kumuunga mkono Mhe rais kwa vitendo.

Kituo hicho kimekamilika na kimeanza kutoa huduma rasmi tarehe 20/01/2023 kikiwa na majengo Nane yaliyojengwa kwa ustadi mzuri ni kituo cha mfano kwakuwa kimetumia fedha kidogo lakini Mjengo yamejengwa mengi na Bora. Majengo yaliyojengwa ni Jengo la wagonjwa wanje (OPD), Jengo la Maabara, Jengo la Mama na Mtoto, Jengo la Upasuaji, Jengo la kufulia, Jengo la Mochwari, kichomea taka na Nyumba ya Mtumishi kwa gharama ya Tsh. 640,206,000/= tu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Ndugu Philemon Magesa amesema kuwa anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuelekeza matumizi ya pesa za mapato ya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi. Hivyo Kutokana na Mji wa Tunduma kufanya vizuri katika Makusanyo ya mapato ya Ndani sasa wamejipanga kuwahudumia wananchi kulingana na Mapato hayo

“Halmashauri ya Mji Tunduma Mpaka sasa tunakusanya mara tatu Zaidi ya kilichokuwa kinakusanywa miaka mitano iliyopita, lazima tutekeleze miradi ya maendeleo iliyo bora ili iwe kielelezo kizuri kwa wananchi kuhusu mapato wanayolipa kuwa nikwa ajili yao na si ya kuwanufaisha wengi, Tunaposema kituo hiki ni cha mfano tunamaanisha ni ubora wa majengo na idadi ya majengo yaliyojengwa ukilinganisha na fedha iliyotumika. Tumezoea kuona Tsh. 500,000,000/= inatumika kujenga majengo 05 lakini sisi Tunduma tumetumia Tsh. 640,206,000/= kujenga majengo 08, ndio maana tunasema kimekuwa cha mfano katika Halmashauri yetu” alisisitiza Mkurugenzi Magesa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Tunduma Dkt. Enock Mwambalaswa amelishukuru baraza la madiwani Pamoja na menejimenti ya Halmashauri ya Mji Tunduma inayoongozwa na Mkurugenzi Philemon Magesa kwa kuamua kujenga kituo hiki huku kikiwa na nyumba ya Mtumishi

 

“Vituo hivi vitasaidia sana kusogeza huduma karibu na wananchi na hivyo kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa mama na mtoto pia kuwepo kwa nyumba hii kutafanya huduma kupatikana muda wote kwani muuguzi atakuwa karibu na kituo hivyo anaweza kufanya kazi muda wowote inapotokea dharura, hata kama sio zamu yake lakini kama kunadharura ya wagonjwa wengi itakuwa rahisi kusaidia na kuokoa wagonjwa” alisisitiza Dkt. Mwambalaswa

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Mhe. Ayubu Mlimba amesema kuwa Baraza lake la Madiwani litahakikisha linapanga, linatekeleza na linajenga miradi ya maendeleo mikubwa Zaidi ya kituo cha Afya

 

“Tangu tumechukua uongozi hapa tumekuwa tukitekeleza miradi mikubwa inayoleta tija kwa wananchi wetu, miradi inayoakisi mahitaji halisi ambayo tuliyaahidi wakati tunaomba watuchague katika kampeni za uchaguzi, hivyo ni jukumu letu kuwatekelezea tuliyowaahidi” asema Mhe. Mlimba

Naye Mwananchi aliyekuja kupata Hudama Bi. Elizabeth Mwashibanda amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali kina mama hususani katika kuwasogezea huduma karibu na makazi yao

 

“Tunamshukuru sana Rais Mama Samia kwa kutujengea Kituoa cha Afya sisi wanawake wa kata ya Chapwa tulikuwa tunahangaika sana tunapopata uchungu wa kujifungua kukodi magari Kwenda Kituo cha Afya Tunduma lakini sasa hapa tutakuwa tunatembea kwa mguu, kwa niaba ya wanawake wa Kata ya Sogea tunasema asante sana mama” alisisitiza Bi. Elizabeth

Sekta ya Afya katika Halmashauri ya Mji Tunduma imekuwa ikikua kwa kasi kubwa kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za Kujenga Hospitali ya Mji Tunduma na Vituo  vya Afya 04 kikiwemo kituo cha Afya Chiwezi, Kituo cha Afya Chipaka ambavyo kinafanya kazi, Kituo cha Afya Mwakakati fedha za tozo ambacho kinafanya kazi na kituo cha Afya Mpande ambacho kipo katika ujenzi. Kwa upande zahanati Halmashauri ya Mji Tunduma ina jumla ya Zahanati 07 kati ya hizo 6 zinatoa huduma na 1 ipo katika hatua za umaliziaji ambayo Rais ametoa Tsh. 86,000,000/= na Halmashauri ikaongeza Tsh. 70,000,000/= kwa ajili ya umaliziaji wake.  

Katika kuhakikisha Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati zote zinafanya kazi vizuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka wa fedha 2021/2022 alitoa Tsh. 376,000,000/= kwa ajili ya kununua Vifaa tiba katika Hospitali ya Mji Tunduma Pamoja na Tsh. 300,000,000/= kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura (EMD)

Hali kadharika katika mwaka wa fedha 2022/2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Tsh. 100,000,000/= kwa ajili ya vifaa vya magonjwa ya kinywa na Tsh. 200,000,000/= kwa ajili ya Vifaa tiba vya Zahanani na Vituo vya Afya.

Kwa kuona umuhimu wa matibabu ya wagonjwa wa mifupa katika Halmashauri ya Mji Tunduma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta mashine mbili za kisasa za Mionzi (Digital X-ray Machine) Pamoja na Mtambo wa Kuzalisha Oksijeni (Oxygen plant) katika Hospitali ya Mji Tunduma.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa