Halmashauri ya Mji Tunduma imeendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita
Shule ya Mwalimu J. K. Nyerere imeendelea kufanya vizuri na kuongeza ufaulu kila mwaka ambapo mwaka 2022 shule hii ilikuwa na watahiniwa 100 kwa Tahasusi mbalimbali, shule hii imefanikiwa kushika nafasi ya 4 Kimkoa na kufaulisha wanafunzi wote walio fanya mtihani wa kidato cha sita
Katika ufaulu wake Shule ya Mwalimu J. K. Nyerere imefanikiwa kufaulisha kama ifuatavyo:-
Daraja la I – 30
Daraja la II – 57
Daraja III – 13
Daraja IV – 0
Daraja la 0 – 0
kwa upande wa shule ya Wasichana ya Mpemba Sekondari nayo imeibuka kidedea kwa kufaulisha wanafunzi wote kwani walikuwa watahiniwa 62 na imeshika nafasi ya 6 kimkoa na kuzibwaga shule kongwe nyingi mkoani songwe
Katika ufaulu wake Shule ya Sekondari Mpemba imefanikiwa kufaulisha kama ifuatavyo:-
Daraja la I – 14
Daraja la II – 44
Daraja III – 4
Daraja IV – 0
Daraja la 0 – 0
Matokeo hayo yametangazwa leo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ambapo watahiniwa wote 162 waliofanya mtihani kwa shule mbili za Halmashauri ya Mji Tunduma wamefaulu.
Ufaulu huu ni kutokana na Jitihada za Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Mhe. Ayubu Mlimba, Mkurugenzi wa Halmamashauri ya Mji Tunduma Bwana Philemon Magesa, walimu wa Shule zote, watumishi, madiwani pamoja na Wazazi wa wanafunzi hao
Akiongea kwa njia ya Simu Mwenyekiti wa Halimashauri ya Mji Tunduma (Diwani wa kata ya mwakakati) Mhe. Ayubu Mlimba amefurahi sana na kusema kuwa
“Motisha tuliyoitoa inafanya kazi, kama Halmashauri ya Mji Tunduma tunatoa Tsh. 10,000/= kwa kila alama A ya somo lolote katika mitihani ya Taifa na kufanya hali ya waalimu kujituma, sasa matunda yake ndio haya yanaonekana” alisema Mhe. Mlimba
Pia Mhe. Mlimba alisema kuwa mshikamano na umoja wa watumishi wa Halmashauri pamoja na uongozi madhubuti wa Afisa elimu sekondari aliye chini ya Mkurugenzi ni chachu ya mafanikio haya
Naye Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mji Tunduma Bwana Philemon Magesa amewapongeza sana walimu na wanafunzi hao kwa matokeo mazuri waliyoyapata kwani yanaifanya Tunduma ing’ae katika Nyanja ya Elimu.
Mkurugenzi Magesa pia alisema kuwa ufaulu huu pia unachangiwa na ujenzi wa miundombinu ambayo inajengwa katika kuhakikisha wanafunzi wa walimu wanapata madarasa na ofisi bora ili kukidhi haja ya kusoma kwa weledi
“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia pesa za UVIKO – 19 za kujengea madarasa na kununua madawati, jambo hilo limepunguza sana msongamano kwa wanafunzi darasani na kuongeza ufaulu” alisema Bwana Magesa
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Bi. Patricia Mbigili amewapongeza sana walimu kwa kushirikiana katika malezi na usimamizi wa masomo kwa wanafunzi wote na kuwataka waendeleze mbinu hizo kwa wanafunzi wengine waliobaki ili Tunduma ije ishike nafasi ya juu kitaifa.
“Kazi yangu kama Afisa Elimu ni kuwaongoza walimu katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi pamoja na malezi, kwa hiyo ufaulu wa wanafuzi wote 162 ni kiashiria kwamba maelekezo na maoini yangu yanazingatiwa ndio maana leo hii tumefika hapa” alisema Bi. Mbigili
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa