• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUNDUMA YAPOKEA MILIONI MIA NNE TOKA SERIKALI KUU UJENZI WA HOSTELI NA MGAHAWA

Imewekwa : April 4th, 2022

Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ujenzi wa awamu ya pili ya Mradi wa Maegesho Tsh. 400,000,000/= za kujenga jengo la nyumba ya kulala wageni (Hostel) na jengo la sehemu ya chakula (Restaurant) ambapo nyumba ya kulala wageni itakuwa na vyumba 20 na mgahawa utakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja 36 kwa mara moja na baa itakuwa na uwezo wa kuhudumia wateje 28 kwa wakati mmoja.

Katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2018/2019, Halmashauri ya Mji Tunduma ili idhinishiwa kutumia fedha kwa ajili ya miradi miwili ya Kimkakati yaani Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka mpaka wa Tanzania–Zambia na Ujenzi wa Stendi ya Mabasi. Mradi wa ujenzi wa maegesho ya magari yanayovuka mpaka wa Tanzania na Zambia upo katika Kata ya Chapwa, mtaa wa Msapania.

 

Mradi huu ulianzishwa kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kuhakikisha kila Halmashauri inaongeza uwezo wa kujitegemea ili kupunguza utegemezi wa fedha toka serikali kuu.

Eneo la ujenzi wa Maegesho lina jumla ya ukubwa wa ekari 17 ambazo Halmashuri ilitwaa kutoka kwa wananchi kwa kuwalipa fidia ili kufanikisha Ujenzi wa Mradi huu pamoja na ujenzi wa ofisi nyingine za taasisi.

Lengo la Mradi huu ni kuiongezea Halmashauri mapato yake ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka Serikali kuu na hatimaye kujitegemea kabisa katika uendeshaji wa shughuli zake. Pia kupunguza msongamano wa malori yanayoegeshwa bila utaratibu kandokando ya barabara.

Halmashauri ya Mji Tunduma ilitengewa fedha jumla ya Shilingi 1,630,000,000.00 kutoka serikali kuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania-Zambia kama mradi wa Kimkakati. Pia katika mapato yake ya ndani ilitenga Shilingi 119,000,000/= kwa ajili ya kulipa fidia ya kutwaa eneo la kujenga mradi huu kutoka kwa wananchi. Hata hivyo mpaka kufikia mwezi Februari 2022 jumla Fedha iliyopokelewa kwa ajili mradi huu ni Tshs 1,936,079,294.00. ambapo ni fedha toka serikali kuu Pamoja na mapato ya ndani.

Tangu kuanza kwa mradi jumla ya Shilingi 1,842,079,294 zimepokelewa toka serikali kuu na Tshs 94,000,000 zimetumika kwenye mradi huu toka mapato ya ndani ya Halmashauri, Hivyo Jumla kuu ni Tshs 1,936,079,294.

Kiasi cha Tshs. 400,000,000 zilizopokelewa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zinaendelea kutumika kwa kujenga nyumba ya kulala wageni (Rest house) pamoja na jengo la mgahawa (Restaurant)

Manufaa ya mradi wa Ujenzi wa Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania–Zambia (Truck’s Parking) ukikamilika unatarajiwa kuiongezea Halmashauri mapato ya ndani na kuongeza ajira kwa vijana hususani katika sekta ya Usafi na Mazingira.

Mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 95 ambapo tayari umeanza kufanya kazi, wastani wa magari 100 yanaegeshwa kila siku.

Mradi huu kwa sehemu iliyokamilika toka imeanza kutumika mwaka 2020/2021 hadi kufikia mwezi Februari 2022 tayari umeingiza kiasi cha shilingi  77,485,300.00. Mapato haya yataongezeka zaidi baada ya kukamilisha awamu hii ya ujenzi wa Nyumba ya kulala wageni na mgahawa.

Mwaka 2021/2022 Halmashahuri ilipokea kiasi cha Tshs 400,000,000 kwa ajili ya kuendeleza mradi huu awamu ya pili, ambapo kwa awamu hii kazi inayofanyika ni kujenga jengo la nyumba ya kulala wageni (Hostel) na jengo la sehemu ya chakula (Restaurant) ambapo nyumba ya kulala wageni itakuwa na vyumba 20 na mgahwa utakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja 36 kwa mara moja na baa itakuwa na uwezo wa kuhudumia wateje 28 kwa wakati mmoja.

Katika ukamilishwaji wa awamu ya pili ya ujenzi, Halmashauri imejipanga kuhakikisha inakamilisha kwa wakati mradi huu, ambapo kwa mujibu wa mkataba kazi hii itafanyika kwa siku 90, kuanzia tarehe 12/02/2022 na kukamilika tarehe 17/05/2022, Kukamilika kwa majengo haya mawili kutawapunguzia adha wateja kwenda mbali kutafuta huduma ya chakula na mahala pa kulala, lakini pia itaongeza mapato ya ndani ya halmashauri ambapo inakadiliwa kupata jumla ya shilingi 75,400,000 kwa mwaka ikiwa hosteli ni shilingi 73,000,000 na restaurant ni 2,400,000

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa