• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUNDUMA YATOA MIKOPO YA 252,422,500/= KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Imewekwa : December 22nd, 2021

TUNDUMA: Naibu waziri OR-TAMISEMI Mhe. David Silinde akiwa mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji mikopo hiyo na alikuwa na haya ya kusema

Napenda kuchukua nafsi hii kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kazi nzuri wanazofanya katika kuhakikisha Maendeleo na Ustawi wa wananchi unafikiwa.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa Halmashauri wa kuviwezesha vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa kuvipatia mikopo yenye masharti nafuu  na  isiyo kuwa na riba. Vile vile nichukue fursa hii kuwapongeza wakuu wa Idara wa sekta za uzalishaji, Maafisa maendeleoya Jamii,MaafisanUstawi wa Jamii na  Maafisa ugani  ngazi za kata kwa kuhamasisha Jamii kuunda vikundi  pamoja kuvisajili ikiwa  ni pamoja na  kutoa miongozo na mafunzo mbalimbali na hatimaye na vigezo vya kuweza  kupata mikopo.

Pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wote walio chini yake  kwa kuona umuhimu wa kuwezesha makundi ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa kuandaa Sheria,Kanuni,Taratibu  na miongonzo mbalimbali inayohusu makundi haya hasa katika kutoa mikopo isiyokuwa na riba na kuwapatia mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli na miradi ya makundi haya ili kujiongezea kipato na kupambana na umasikini.

Nafurahi kusikia  na nimeona kwa macho kwamba mikopo hii imewafikia wananchi walio wengi na itasaidia kuinua hali za kiuchumi kwani walengwa wa mikopo hii mtaboresha shughuli zenu za uzalishaji mali na kujiongezea kipato kwa kutumia ipasavyo  mikopo hii .

Ni matarajio yangu kuwa  mikopo  hii  itatumika  kama  ilivyotarajiwa ili kuweza kufikia malengo yenu mliojiwekea sambamba na utekelezaji wa Sera  ya  Maendeleo  ya  Jamii  na  utekelezaji  wa  Ilani ya Chama  cha  Mapinduzi  (CCM)  ya Uchaguzi  Mkuu  wa mwaka 2020, Lengo  ni kuwawezesha wananchi kiuchumi ili kujiletea maendeleo endelevu.

Inayotutaka kuhakikisha wananchi wanawekewa mazingira mazuri ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za Maendeleo, ni pamoja na kuwapatia mitaji wanawake, vijana na watu wenye ulemavu

kupitia mikopo yenye masharti nafuu, kuwezesha vijana, wanawake na makundi mengine ya wajasiriamali kujiajiri.

Pia naomba nichukue fursa hii kuwapongeza wanavikundi mlio bahatika kupata mikopo kwa miaka ya nyuma toka utaratibu huu ulipoanzishwa na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo kwa vikundI , pia nimetaarifiwa kuwa  Siku ya leo mikopo yenye thamani ya shilingi 252,422,500/=  inatolewa kwa vikundi vya wanawake 9 shilingi 121,000,000.00 vikundi vya vijana 4 shilingi  99,000,000.00 na  kwa  watu wenye ulemavu 6  shilingi 32,422,500.00

 Fedha hizo zinakwenda kutekeleza ukuzaji wa mitaji , uchumi na ununuzi wa vifaa na vyombo vya usafiri katika ngazi  za  vikundi  kwa kutekeleza miradi ainishwa ambayo ni shughuli za usafirishaji (bodaboda na bajaji), uongezaji mnyororo wa thamani,utengenezaji wa Batiki, Sabuni za maji na miche ,ununuzi wa nafaka, ufugaji wa kuku na Ng’ombe, ununuzi  na uuzaji  na usafirishaji wa Samaki wakavu, ukoboaji na uuzaji  mchele, ununuzi na  uuzaji viazi mviringo na matunda, utengenezaji vifungashio (bahasha), uuzaji mahitaji ya nyumbani na utengenezaji wa keki, uboreshaji wa duka la Nyama,uboreshaji wa saloon ambapo shughuli hizo nimeziona hapo nje nilipokagua shughuli za vikundi nawapongeza sana kwa jitihda hizo zilizoanza kuonekana.

Fedha hii mkaitumie kama mlivyoomba na nimesikia  wengine tayari mmeshanunua Vifaa na bidhaa kwa ajili ya miradi yenu ili kujiongezea kipato, ninaamini kuwa vikundi hivi vimechaguliwa kwa kuzingatia vigezo muhimu vilivyopo kwenye Sheria ,Kanuni na miongozo ya utoaji wa mikopo hii.

Hivyo basi ni matumaini yangu mikopo hii mnayoipata leo itaanza kurejeshwa kwa kufuata utaratibu mliowekewa na kuzingatia vipengele vyote vilivyosainishwa kwenye mkataba wa mikopo hii.

Kumbukeni kuwa mikopo hii sio Zawadi na wala siyo Fedha za kwenda kugawana hivyo basi ni vema ikarejeshwa kwa wakati ili kuwawezesha wanavikundi wengine kunufaika na mikopo hii. Vilevile sitegemei kuona kikundi chochote kinachukuliwa hatua za kisheria kutokana na kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati. Iwapo kitatokea kikundi   kitavunja makubaliano  ya  kwenye  mkataba  kikundi  kitafikishwa  kwenye vyombo vya Sheria  kama sheria inavyosema atakayetumia fedha za Mkopo uliotolewa chini ya kanuni hizi kwa matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Kamati ya Fedha na Utawala au atakayetoa taarifa za uongo kwa lengo la kujipatia mkopo huu atakuwa ametenda kosa na endapo atatiwa hatiani atatozwa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na kisichozidi shilingi milioni moja au kutumikia kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa