• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUNDUMA YATOA TUZO ZENYE THAMANI YA MILIONI THELATHINI NA NNE KATIKA KILELE CHA JUMA LA ELIMU

Imewekwa : May 7th, 2022

TUNDUMA: SONGWE

Halmashauri ya Mji Tunduma imetoa Tuzo kwa SHULE BORA, WALIMU HODARI NA WANAFUNZI HODARI katika mitihani ya Taifa ya DARASA LA NNE, DARASA LA SABA, KIDATO CHA PILI NA KIDATO CHA NNE kwa mwaka 2021 kwa kugawa zawadi jumla ya Tshs. 32,400,000/=

Akisoma taarifa mbele ya Mgeni Rasmi Mhe. Dvid Silende (Mbunge) Naibu waziri OR-TAMISEMI ameeleza kuwa mpaka sasa Halmashauri ya Mji Tunduma  ina jumla ya shule 63 kutoka shule 26 za mwaka 2016. Ongezeko hili kwa miaka 7 ni sawa na 142%, Kati ya shule hizo shule 49 ni za Serikali na 14 ni Binafsi. Jumla ya wanafunzi katika Shule za Serikalini 45,848 ikiwemo wavulana 22,615 na wasichana 23,233. Idadi ya wanafunzi shule Binafsi 2494, hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wote kwa Shule za Serikali na Binafsi kuwa 48,342.

Kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inasisitiza kuwa kila shule ya Msingi ni lazima iwe na darasa la Elimu ya Awali kwa Lengo la kumuandaa mtoto kabla ya kujiunga na Elimu Msingi. Halmashauri imeendelea kusisitiza hilo hivyo shule zote 63 zina wanafunzi wa darasa la Awali wapatao 4,102 ikiwa shule za Serikali kuna wanafunzi 3,746 na shule za Binafsi kuna wanafunzi 356.

Aidha kwa upande wa uandikishaji kwa wanafunzi wa darasa la kwanza mwaka huu 2022 walitarajiwa kuandikishwa wanafunzi 5,790 walioandikishwa ni wanafunzi 6,527 sawa na 113%.

Kwa ujumla Mji wetu unaendelea kukua kwa kasi kubwa sana na hivyo kila mwaka kuna ongezeko kubwa sana la wanafunzi wanaoandikishwa darasa la Awali na la Kwanza ukilinganisha na wanafunzi wanaohitimu darasa la saba

Pamoja na upungufu huo wa miundombinu Serikali yetu chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na usimamizi wako imeendelea kutoa fedha mwaka hadi mwaka ili kupunguza changamoto ya miundombinu.

Mwaka huu tumetekeleza miradi mikubwa ifuatayo;

  • Ujenzi wa shule mpya 2 ambazo ni Shule ya Msingi Kokoto Tshs.400,000,000 na Shule ya Msingi Melelani Tshs.250,000,000
  • Fedha za EP4R ambazo zimejenga Mabweni mawili ya watoto wenye mahitaji maalum, kila bweni liligharimu kiasi cha Tshs.80,000,000 hivyo kufanya jumla ya Tshs.160,000,000
  • Fedha za EP4R Tshs. 559,200,000 ambazo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
  • Fedha za LANES Tshs. 163,395,000 ambazo zilitumika kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vya madarasa. Hata hivyo tumeendelea kutumia fedha za mapato ya ndani zaidi ya Bilioni mbili kwa mwaka 2021/2022 kujenga na kukamilisha miundombinu ya vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo. Tunawaomba wadau wa Elimu waendelee kuunga mkono jitihada za Serikali juu ya kutatua tatizo la miundombinu inayohitajika shuleni.

Hali ya kitaaluma kwa Halmashauri ya Mji Tunduma imekuwa ikipanda mwaka hadi mwaka na tunawashukuru sana walimu wote na wadau mbalimbali kwa ushirikiano na juhudi zao kwani ndizo zinapelekea ufaulu huo kupanda kwa darasa la VII na la Nne

Halmashauri ya Mji Tunduma ina shule za Sekondari 19 kati ya hizo shule za serikali ni 14 na 5 za Binafsi. Tunaishukuru sana Serikali na wananchi kwa ujumla kwa ujenzi wa shule katika kipindi kifupi kwani mwaka 2016 kulikuwa na shule 6 tu za Sekondari na kati ya hizo 5 zilikuwa za serikali na Moja tu ya Binafsi. Idadi ya Wanafunzi hadi sasa kwa shule za serikali jumla ni 9,320 wavulana 4,339 wasichana 4,981 na wanafunzi wa shule za Binafsi wapo 924 wavulana 396 na wasichana 528. Wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 katika Halmashauri ya Mji Tunduma walipata nafasi kwa asilimia mia moja. Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na wewe Mhe.Mbunge,Waheshimiwa Madiwani na Wananchi kwa ujumla kwa kutoa ushirikiano katika kujenga madarasa ya kutosha kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi hawa. 


Kwa ujumla mahitaji ya walimu wa Sekondari ni 355 na waliopo ni 235 na upungufu ni 120. Upungufu mkubwa ni kwa masomo ya Sayansi na Hisabati

Tunakuomba sana kutusaidia kupata walimu watakaoajiriwa kupitia nafasizilizotangazwa na Serikali hivi karibuni ili kupunguza uhaba mkubwa tulionao.

Halmashauri kwa sasa haina upungufu wa vyumba vya madarasa hii ni baada ya Serikali kujenga madarasa mengi kupitia Mradi Na TCRP 5441. Kwa mara ya

kwanza Halmashauri ina ziada ya vyumba vya madarasa tofauti na miaka iliyopita hapa tuna kila sababu ya kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,wewe Mhe.Mbunge na Waheshimiwa Madiwani kwa kushirikiana na wananchi kujenga miundombinu ya Mwezi Oktoba, 2021 Halmashauri ilipokea jumla ya Shilingi 1,040,000,000 kupitia

mradi wa COVID 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 52 katika shule za Sekondari. Miradi yote ilikamilika kwa wakati tayari madarasa yanatumika. 

Katika utekelezaji wa Programu ya Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Halmashauri imepokea fedha za ujenzi wa shule mbili ikiwemo shule ya Wasichanaya Mkoa ya Kitaifa inayojengwa kata ya Chiwezi Mtaa wa Namole. Shule hii imetengewa Tsh. 4,000,000,000/= na zimepokelewa Tsh.3,000,000,000/=.Tayari mradi umeanza kutekelezwa. Shule ya pili ni Uwanjani Sekondari ambayo

imepokea Tsh.470,000,000/= na kazi za ujenzi zinaendelea.

Hali ya taaluma kwa Halmashauri imeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka kwa viwango tofauti tangu mkoa ulipoanzishwa mwaka 2016. Matokeo yote ya mitihani ya Kitaifa kuanzia Upimaji wa kidato cha Pili, Mitihani ya Taifa kidato cha Nne na cha Sita yote yanaimarika mwaka hadi mwaka kama ifuatavyo:-

                Mwaka  2020 Mwaka    2021

1 Kidato cha Pili  98.7%              99.4%

2 Kidato cha Nne 95.4%             99.2%

3 Kidato cha Sita 99.3%             100%

Aidha, kwa mwaka 2021 ufaulu uliimarika zaidi hasa kwa kidato cha Nne na Halmashauri ya Mji Tunduma ilishika nafasi ya 6 Kitaifa na imepata tuzo ya kuwa miongoni mwa Halmashauri zilizoongeza ufaulu mfululizo kwa miaka 03 kuanzia mwaka 2019, 2020 na 2021. Waheshimiwa Madiwani na kupitia Baraza la Madiwani lililofanyika tarehe 29.10.2022 waliazimia kutoa tuzo kwa walimu pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya Kitaifa.

Nichukue nafasi hii pia kukupongeza Mgeni Rasmi kwani ujio wako katika tukio hili litatoa hamasa kubwa kwa wanafunzi, walimu pamoja na jamii katika kuboresha ufaulu kwa watoto wetu. Halmashauri kwa kushirikiana na Mkoa imeweka mikakati endelevu inayotekelezeka.


Tuzo zimegawanyika katika makundi mbali mbali kama ifuatavyo:-

i) Shule zenye ufaulu wa asilimia miamoja

ii) Shule zenye wastani mkubwa wa ufaulu (GPA)

iii) Shule zilizoongeza ufaulu wa daraja la kwanza

iv) Walimu waliofanya vizuri kwa kila somo

v) Ufaulu wa alama “A” kwa kila somo

vi) Wanafunzi waliofanya vizuri kiujumla


Kwenye mafanikio lazima changamoto ziwepo, zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazotukabili kwenye sekta ya elimu

1. Baadhi ya shule kutotoa chakula cha mchana kwa wanafunzi

2. Baadhi ya wanafunzi kujihusisha na biashara ndogondogo , hali inayopelekea

kutozingatia masomo.

3. Utoro wa rejareja wa baadhi ya wanafunzi.

4. Baadhi ya wazazi kuwakataza watoto wao kufanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa.

5. Mrundikano mkubwa wa wanafunzi madarasani kwa shule za Msingi

6. Uhaba wa walimu.

UTATUZI WA CHANGAMOTO

  1.  Kupitia baraza la madiwani tumetunga Rasimu ya sheria ndogo ya utoaji wa chakula cha mchana shuleni ambapo Rasimu hiyo imeshawasilishwa OR [1] TAMISEMI.
  2. Elimu imeendelea kutolewa kwa wazazi wanajamii ili kuweza kuacha kuwatumia wanafunzi kwenye biashara ndogondogo
  3.  Tumeendelea kutoa Elimu kwa wazazi na walezi ili kuweza kukomesha utoro wa rejareja
  4.  Aidha tumeendelea kuwahamasisha wazazi /wanajamii juu ya umuhimu wa Elimu tunakushukuru mgeni Rasmi kwa mwaka huu uliamua kuwashonea Sare wanafunzi wote wa Shule ya msingi Chiwezi waliofaulu kwa asilimia100. katika mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi. Kwani wazazi wao walikuwa ni miongoni mwa wazazi waliokuwa wakiwataka watoto wao kutofanya vizuri kwenye mitihani ya kuhitimu darasa la VII.
  5.  Kutokana na uhaba wa vyumba vya Madarasa tumeendelea kuhamasisha jamii juu ya kujitolea nguvu kazi yao ili kutatua changamoto hiyo na kuvitumia vyumba vichache vilivyopo.
  6.  Pia tumeendelea kuwa na walimu wa kujitolea ambapo mpaka sasa tuna jumla ya walimu 48 wanajitolea kwenye shule zetu.

MIKAKATI YA KUONGEZA UFAULU

  1.  Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji ngazi ya Kata na Shule ili kuinua taaluma na kuongeza ufaulu
  2.  Kufanya mitihani ya mapoja ya mwisho wa mwaka kwa darasa la sita, Kidato cha Kwanza, tatu na cha tano ili kuwapima kabla hawajaingia madarasa ya mitihani.
  3.  Kudhibiti utoro wa walimu shuleni na madarasani.
  4.  Maafisa Elimu Kata kuwasilisha taarifa za ufuatiliaji na usimamizi kila mwezi
  5.  Kuzifanyia kazi taarifa za Wathibiti wa Ubora wa Shule kwa wakati ili kuongezatija katika utendaji

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa