• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUTOKE ENZI ZA KUUZA NG'OMBE KWA KESI YA KUKU_RC KINDAMBA

Imewekwa : February 2nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia elimu waliyoipata wakati wa maadhimisho ya wiki ya Sheria iwasaidie kupata suluhu ya migogoro katika jamii huku akiwaasa kutoka zama za kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku.


RC Kindamba ametoa rai hiyo leo Jumatano Februari mosi, 2023 wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Songwe iliopo Nselewa.


Amesema kuwa kupitia maadhimisho hayo wadau wa mahakama watawaongoza wadaawa ambao ni mshtaki na mshtakiwa katika kutatua mgogoro wao kwa njia ya usuluhishi.


"Ni matumaini yangu watu wa mahakama na wananchi wa Mkoa wa Songwe wameyatendea haki maadhimisho ya wiki ya Sheria mpaka kufikia leo kilelele cha maadhimisho hayo kwa kujitokeza kupata elimu na kufahamu hatua mbalimbali za kufungua majalada mahakamani" amesema mkuu huyo wa mkoa.


Katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu: wajibu wa mahakama, RC Kindamba ametoa wito kwa jamii kutafuta njia bora za utatuzi wa migogoro na si kuendeleza zilizopitwa na wakati.


"Tutoke katika enzi za kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku, lazima tutafute suluhu ya migogoro yetu" amesesitiza mkuu huyo wa mkoa


Ameeleza kuwa Rais Samia anatamani watanzania wote wapate haki na kuwataka waliopewa dhamana ya kuwasimamia wananchi watende haki.


Akisoma hotuba kwa mgeni rasmi Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Hassan Makube amesema mahakama ina jukumu la kuhakikisha kuwa suala la utoaji haki linafanyika kwa wakati.


Makube amezitaja changamoto za kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kuwa ni uelewa mdogo wa njia hiyo, kutokuwa tayari kujishihusha na gharama ya kuwalipa wasuluhishi nje ya mahakama.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba, Fakii Lulandala ambaye amekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amesema kuwa katika moja ya jukumu la ofisi ya mkuu wa wilaya ni usuluhishi wa migogoro hivyo ofisi hiyo inapunguza kesi mahakamani.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa